Friday, 14 November 2008

Ben R. Mtobwa afariki!!

Poleni sana wafiwa.
Mimi ni mmoja wa wasomaji wa vitabu vya Ben.

Salaam za Mhe Rais wa Jamhuri ya Muungano:
............................................................

DIRECTORATE OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS

UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
Telephone: 255-22-2114512, 2116898

E-mail : press@ikulu.go.tz

Fax: 255-22-2113425

PRESIDENT’S OFFICE,
THE STATE HOUSE,
P.O. BOX 9120,
DAR ES SALAAM.
Tanzania.

Ben Mtobwa alikuwa mwanataaluma mzalendo

RAIS Jakaya Mrisho Kikwete ametuma salamu za rambirambi kwa familia ya mwandishi wa habari na vitabu maarufu nchini, Ben Mtobwa, aliyefariki dunia Jumapili iliyopita, Novemba 9 2008, mjini Dar Es Salaam.
Rais amemwelezea marehemu kama mwanataaluma mzalendo ambaye aliitumia kalamu yake kwa busara na kwa ajili ya kuleta maelewano ndani ya jamii ya Tanzania.
Katika salamu hizo, Rais Kikwete ameieleza familia hiyo: “Naungana nanyi wote katika wakati huu mgumu na wa majonzi makubwa mliyonayo kwa msiba huo mkubwa uliowapata. Tunaelewa machungu mliyonayo”
Amesisitiza Rais Kikwete katika salamu hizo za rambirambi: “Nimemjua marehemu Mtobwa kwa miaka mingi katika ujenzi wa taifa letu, hususan katika masuala yaliyohusu utaalamu wake wa masuala ya habari na uandishi.”
“Marehemu Mtobwa alikuwa wanataaluma mzalendo, aliyetumia kalamu yake kwa busara na kwa nia ya kuleta maelewano ndani ya jamii yetu. Alijali maadili ya taaluma yake na kutimiza vyema wajibu wake katika jamii kwa mujibu wa maadili hayo.”
Amemalizia Rais Kikwete: “Naungana nanyi wote katika kuomboleza msiba huu mkubwa. Kwa pamoja tumshukuru Mungu kwa kumwezesha Ndugu Mtobwa kutoa mchango wake kwa taifa letu.”
Marehemu Mtobwa anatarajiwa kuzikwa leo kwenye shamba lake Bunju A mjini Dar Es Salaam.

Mwisho

Imetolewa na Kurugenzi ya Mawasiliano

Ikulu.
Dar es Salaam.
12 Novemba, 2008
(source: the united republic of tanzania official website)

No comments: