Saturday 29 March 2008

TAMWA miaka 20 leo

* SOURCE: Nipashe, 29 Mar 2008

Wanachama wa Chama cha Wanawake Wanahabari (TAMWA) leo wanaadhimisha miaka 20 ya kuzaliwa kwa chama hicho kilichoasisiwa mwaka 1987. Maadhimisho ya siku ya kusherehekea mafanikio ya TAMWA, yanaanza asubuhi hii katika ofisi zake mpya zilizoko Sinza Mori, jijini Dar es Salaam. Mke wa Rais, Mama Salma Kikwete, anatarajiwa kuwa mgeni rasmi.
Taarifa iliyotolewa na TAMWA jana ilisema, Mama Kikwete ataweka jiwe la msingi la ofisi hizo pamoja na kuongoza shughuli za kutunisha fedha za ujenzi wa maktaba ya kisasa ya chama hicho utakaogharimu zaidi ya Sh. milioni 60. Wadau mbalimbali wakiwemo marafiki na washirika wa TAMWA wa ndani na nje ya nchi, watajumuika pamoja kuwaenzi waasisi, kushangilia mafanikio na kuchangia ujenzi.
``TAMWA imefanya masuala mengi, kuhimiza usawa wa jinsia, kupinga mila potofu za kukandamiza wana jamii, kupinga utumikishaji watoto, ndoa za utotoni, kupiga vita rushwa, kuhimiza kuongeza ushiriki wa wanawake kwenye uongozi na katika ngazi za maamuzi,`` ilisema sehemu ya taarifa.

No comments: