Tuesday 19 February 2008

Ukarimu wa Bush umenigusa

Jamani Rais wa Marekani amenigusa sana kwa jinsi alivyotujali na kutuheshimu watanzania.
Kuanzia ukarimu na ucheshi wake hadi misaada aliyoitoa kwa nchi yetu. Hasa lengo lake ni kuwasaidia wanyonge.
Ningependa kuona hizo fedha alizoahidi kutusaidia zinaelekezwa kule kulikotarajiwa. Wahusika kazi kwenu.
Misaada hiyo kama ilivyoripotiwa ni;

1. Dola za Marekani milioni 698 (zaidi ya sh. bilioni 700) chini ya Mpango wa Changamoto za Milenia (MCC)* kwa ajili ya kusaidia miradi mbalimbali ikiwemo ya kutokemeza malaria, UKIMWI na kuimarisha miundombinu.
Mbali na kusaidia kusaidia kutokomeza magonjwa hayo pesa hizo zitasaidia kuimarisha miundombinu ya barabara na sekta ya nishati ambapo kati ya fedha hizo,jumla ya dola 206 zitashughulikia upatikanaji wa umeme na dola 166 zitaelekezwa kuhakikisha upatikanaji wa maji safi na salama.

Msaada huo ni wa aina yake kwani haujawahi kutolewa na Marekani kwa nchi yoyote kwa wakati mmoja na unatarajiwa kunufaisha zaidi ya Watanzania milioni 4.8

Pesa zilizotolewa jana, zinaweza kujenga viwanja 12 vya michezo vya kisasa mithili ya ule wa Taifa uliojengwa hivi karibuni, jijini Dar es Salaam kwa gharama ya sh. bilioni 56.

Sambamba na Tanzania, nchi zingine zitakazonufaika na msaada wa Marekani ni Benin iliyopata dola milioni 307, Rwanda itakayopata dola zaidi ya milioni 17, Ghana dola milioni 547 na Liberia dola milioni 156.


2. vyandarua milioni 5.2 kama sehemu ya kampeni yake ya kupambana na malaria Afrika, Kusini mwa Jangwa la Sahara.

Rais Bush alitangaza mpango wake huo jana katika hospitali moja jijini hapa jana katika siku yake ya tatu ya ziara yake katika nchi tano za Afrika.

Alisema nchi yake itahakikisha kila mtoto wa Tanzania mwenye umri wa mwaka mmoja hadi mitano, anapata chandarua.

Malaria ni chanzo kikuu cha vifo kwa watoto barani Afrika na inaua mtoto kila baada ya sekunde 30, takwimu za Umoja wa Mataifa zinasema.

Marekani, Tanzania na Mfuko wa Dunia wa Kupambana na UKIMWI, kifua kikuu na malaria, ndio watakaosimamia usambazaji wa vyandarua hiyo.

"Hii ni moja ya teknolojia rahisi, lakini inayofanya kazi sana," alisema Rais Bush baada ya kutembelea hospitali ya wilaya ya Meru, Arusha jana.

"Ni jambo lisilokubalika kwa watu katika Afrika, kuona familia zao zikiangamia na uchumi kudorora.

"Haikubaliki kwa watu nchini Marekani ambao wanaamini kuwa maisha ya kila mtu yana thamani na kwamba uwezo wa kuokoa maisha unatokana na dhamira ya dhati," alisema.

*MCC - Millenium Challenge Cooperation
(by mosonga with news extracts from www.majira.co.tz)

No comments: