Tuesday 18 September 2007

Nyasi bandia Tanzania wapi na wapi!

Kwanini lakini nyasi bandia???
Mengi nilishayasema kuhusu hizi nyasi bandia. Leo sitasema zaidi, ila nasema tena Tanzania hatuhitaji kamwe kuwa na viwanja vyenye nyasi bandia!
Hizo hela zingetumiwa kufundisha walimu wa michezo (mpira wa miguu) ktk ngazi za wilaya na vijiji ili tupate kisima cha wachezaji tokea vijijini hadi mijini kwa ajili ya timu zetu na hasa timu ya Taifa.
Hivi kweli TFF imeenda FIFA kuomba mamilioni ya hela kwa ajili ya kutandaza nyasi bandia toka nje ya nchi, kununua mchanga nje ya nchi madawa ya kutunza 'nyasi' na wataalamu wa kuzitandaza halafu kila miaka 5 hadi 10 tulipie wataalamu wa kufanya mategenezo!
Kisa ni nini hasa? Au ina maana nyasi za asili hazioti au kukua Tanzania?
Na Mosonga

2007-09-18 13:45:10
By ITV Habari
Wataalam wa kutandaza nyasi bandia katika uwanja wa taifa wa zamani na ule wa karume walitarajiwa kuwasili nchini jana kwa ajili kusimamia zoezi hilo litakalo kamilika baada ya siku kumi.

Afisa habari wa shirikisho la soka Tanzania - TFF, Florian Kaijage, amesema wataalam hao ambao wanatoka Uholanzi wamepewa kazi hiyo na shirikisho la kandanda Duniani- FIFA, na watashsirikiana na mkandarasi wa hapa nchini.
source: alasiri

No comments: