Tuesday 9 December 2008

Mipango na Makazi

Zipo aina nyingi za mpangilio ya makazi (forms of settlements).
1. Linear
2. Grid
3. Radial
4. Clusters

Pia ipo sera ya serikali (wizara ya ardhi) kuhalalisha maeneo yasiyo rasmi (squatters) ili yapewe hati rasmi na kutambulika kisheria.
Ipo mifano mingi duniani ambapo makazi yasiyo rasmi huhalalishwa (na kutambulika) kisheria.
Baada ya uhalalishwaji wa maeneo hayo, huduma muhimu za kimaisha husambazwa huko, mathalani;
-barabara inayopitika majira yote,
-huduma za maji, umeme n.k.

Mipangilio ya makazi ipo ya aina nyingi kama ilivyoonyeshwa hapo juu. Kwa hiyo sio lazima mpangilio wa ujenzi wa makazi uwe ktk mstari ulionyooka kama wengi wanavyodhani. Inaweza kuwa "organic, random, cluster or even contrasting shapes". Usanifu unatoa nafasi ya kufanya uzuri uonekane ktk maumbile mengi, sio mstari ulionyooka kama tulivyozoea!

1 comment:

MOSONGA RAPHAEL said...

Yafuatayo ni maoni juu ya mada ya Makazi na Mipango Miji yaliyotolewa na wasomaji mbalimbali wa Blog ya Michuzi:

Mpangilio wa UJENZI wa Nyumba Bongo bado sio TAMBARARE.... Hapo ukiangalia haraka haraka ingewezekana kujenga Nyumba Nyingi zaidi Kama Nyumba zingekuwa na mpango mzuri lakini kwa kuwa kila nyumba imejengwa kutokana na Matakwa ya Mjenzi, Inaonekana kama ni VIPANYA(HIACE) vimepanga Magomeni kusubiria Bingo.
Kama kawaida Mchango wangu,
B. Mbakiaji


Tarehe December 06, 2008 8:45 PM, Mtoa Maoni: Anonymous
Mbona Mugabe alichukua hatua madhubuti kwa vitu kama hivi mkaanza kumalumu? Bomoa bomoa ikipita mnalaumu. Mipango miji ipo na sheria zipo, ukiangalia kwenye karatasi miji yetu mingi inapendeza ila hali halisi ndiyo hiyo. Siasa zimezidi sana afrika.


Tarehe December 06, 2008 8:57 PM, Mtoa Maoni: Anonymous
Ukweli unauma.


Tarehe December 06, 2008 9:03 PM, Mtoa Maoni: Anonymous
HAYA YALIANZIA WAKATI WA AWAMU YA KWANZA YA URAISI.
HAYAKUWEPO WAKATI WA UKOLONI CHINI YA SERIKALI YA KIINGEREZA.


Tarehe December 06, 2008 9:37 PM, Mtoa Maoni: Anonymous
kifupi bongo bado! ila ubishi tunao. kwa sbbu ukweli ni kwamba ukitaka maendeleo jilinganishe na aliye juu yako kimaendeleo na siyo unajilinganisha na wachini yako.
jibu ziro


Tarehe December 06, 2008 9:38 PM, Mtoa Maoni: Anonymous
ni aibu ndugu yangu.inasikitisha viongozi wetu wanavyofanya kazi bila hata kuchungulia wenzao wanafanya nini. Hakuna uwajibikaji kabisa


Tarehe December 06, 2008 9:39 PM, Mtoa Maoni: Anonymous
Je tuwavunjie nyumba hao wote waliojibanza hapo, au tutafute namna ya kuzuia watu kujenga hovyo kwa ku waelimisha zaidi kuhusu sheria za aridhi na kuweka wazi plan iliyopo ya jiji la Dar??
Mdau namba 6


Tarehe December 06, 2008 10:53 PM, Mtoa Maoni: Anonymous
mie naunga mkono ramani zipo zak ujengwa nyumba kwa mistari na ni sheria ila wajumbe ma diwani wanakula pesa nyumba zijengwe tu ovyo na wananchi wanajuwa baada muda zitavunjwa wana jenga, alafu wanasema serikali siyo ya kulaumiwa vipi si yakulaumiwa? wakati wanawacha tu watu wajenge ovyo bila mpangilio? lazima wawekwe kiti moto kwenye tv live waulizwe wajibu.


Tarehe December 06, 2008 11:01 PM, Mtoa Maoni: Anonymous
SASA UNATAKA KUSEMA NINI? NYUMBA SI LAZIMA ZIWE KWENYE MSTARI ULIONYOKA, KWANI HUO NI UKALE, KINACHOTAKIWA NYUMBA ZIWE SAFI ZA KISASA, NA BORA KWA AFYA NA MATUMIZI YA BINADAMU PIA KUWE NA ACCESS YA KUINGIA NA KUTOKA ZILIPO, HATA HUKO KENYA KUNA NYUMBA ZA MPANGO HUO TENA AFADHALI YA SISI WAO NI MABATI TU YALIOOKOTWA JALALANI NA KUTENGENEZA NYUMBA ZA MADANGE, THEY ARE JUST MAKSHIFT HOUSES UNFIT FOR HUMAN BEING, VINYESI VIKITIRIRIKA OVER THE LAND, HALI YAO NI MBAYA WEWE ACHA TU, TANZANIA TUKO JUU SANA SOCIALLY AND STANDARD OF LIVING TUKILINGANISHWA NA WAO, PENGINE HAMJAFIKA KENYA NENDENI MKAJIONE WENYEWE.


Tarehe December 06, 2008 11:29 PM, Mtoa Maoni: Anonymous
hawa jamaa wamejenga nyumba nzuri tu ila hakuna wa kuwapimia viwanja na kuwaelekeza namna wanavyotakiwa kujenga ila uwezo wameonyesha wanao. ndungu yangu hata hao watani wetu mambo haya wanayo tusiwakweze sana


Tarehe December 07, 2008 12:03 AM, Mtoa Maoni: Anonymous
Twende mbele turudi nyuma lakini watanzania tumechemsha vibaya sana kwenye mipango mji. Anyway ni muda muafaka kuwawajibisha wazembe na kuweka watendaji wenye vision na uzalendo wa kuendeleza nji hii!


Tarehe December 07, 2008 12:54 AM, Mtoa Maoni: Anonymous
Huoni hata kaka michuzi anashauri kutolewe barabara sijui wapi kule kupunguza traffic?
Survey hamna bongo just your idea siku zinaendelea na baba kukatia kiwanja mwanae papo kwa papo. halfu ukiengezea na family cemeteries basi tena hamna cha mipango miji wala nini. Ukitaka kufika kwangu ni yaleyale karibu na mnazi , nyuma ya golden rose ouch.....That will never change in million years


Tarehe December 07, 2008 1:30 AM, Mtoa Maoni: Anonymous
Hapo kutafuta anwani ni issue especially kwa cc wabeba mabox, ambulance itapita wapi?Alley ndo ipi na main road ndo ipi usinipe jibu.


Tarehe December 07, 2008 1:35 AM, Mtoa Maoni: Anonymous
Sasa wewe kinachokuuma nini tumboni yakhe...si nyumba tuu...kwani ulitaka binadamu waishi jini ya makuti!!!???ahh nyie wabeba maboksi wala hamridhiki na mna vivu wa taifa langu!


Tarehe December 07, 2008 1:54 AM, Mtoa Maoni: Anonymous
Sasa mjomba si kila mtu anajenga kuelekeza dirisha upepo unakotokea ili atape japo kajihewa ka kumfanya alale usiku.!!?? hehehehe


Tarehe December 07, 2008 2:19 AM, Mtoa Maoni: Anonymous
Pengine, miji yetu hukua wakati wa usiku wakina afisa mipango miji, diwani, mbunge, mkuu wa wilaya, na mkuu wa mkoa wote wamelala! Au, mji kwanza ndipo hao wajamaa wanaandikwa kazi! Ni nani alifikiria miaka ya 1970s kwamba Kimara na Makongo itakuwa ni sehemu ya Jiji la Dar es Salaam?
Hata sehemu za " national urban housing schemes" za Magomeni, Mwananyamala na Kinondoni, japo zilijengwa kwa misaada ya Ujerumani, barabara zake hazikuwa za kupimwa, kitaalam!


Tarehe December 07, 2008 2:51 AM, Mtoa Maoni: Anonymous
Hiyo kweli kabisa, wanakula pesa za watu na kazi ya maana haionekani. Ila baada ya muda, utasikia wanataka kupanua barabara, mara nyumba zinabomolewa na fidia zenyewe za kusumbua. Au sa nyingine wanakulipa fidia ya kiwanja kwa bei ya miaka hiyo ya nyuma wakati sa ivi gharama za maisha zimepanda mara alfu.
It definately needs looking at!


Tarehe December 07, 2008 3:10 AM, Mtoa Maoni: Obwatasyo Impokochole
Kutoka juu mimi nimeweza kusoma kupitia huu mpangilio wa majengo maandishi ya :
'Menemene Tekeli na Peresi!'


Tarehe December 07, 2008 12:00 PM, Mtoa Maoni: Anonymous
Bro Michu na wadau hapa bila shaka ni tabata kule maeneo ya kisukulu ama karibu na hapo, correct me if am wrong na inaonekana nyumba zote sio za nyuma ya 1995. Kweli jiji linapanuka kwa kasi na bila mpangilio


Tarehe December 07, 2008 12:43 PM, Mtoa Maoni: Anonymous
Wewe anonymous wa 06, 2008 11:01 PM inaonekana kwa ligi ndio mwenyewe.Wakati ulipokuwa mdogo ulikuwa unabishana mpaka na taarifa ya habari wewe. Utake usitake Tanzania mipango miji yetu ni mibovu. Wa kulaumiwa ni wote serikali na wananchi. Mfano mdogo tu; mtu unauziwa kiwanja,anayekuuzia anakwambia acha hatua tatu pembeni kwaajili ya barabara, wewe unagoma unajenga mpaka sehemu iliyotengwa kwa ajili ya barabara. Unategemea nini?.Je wenzio wote wangejenga mpaka barabarani wewe ungefikaje hapo unapojenga?.Hou ni ukosefu wa busara ya kawaida kabisa ambayo haihitaji hata kwenda shule. kuanza kushupaa na kutupa madongo Kenya hakusaidii kitu hapa.Hata kama wakenya wana tatizo kama hili hujui wanafanya nini kulitatua hapo mbeleni.Cha msingi ni sisi upande wetu kushinikiza watu wawe wastaarabu na serikali yetu ifanye kazi yao na sio kupokea mishahara ya bure.
Mdau
Cardiff


Tarehe December 07, 2008 12:52 PM, Mtoa Maoni: Anonymous
Nyie wote huko juu mnajifanya kama vile hamjui hali halisi, kama vile hamjawahi kuona squater hao hamtoki kwenye squater, ina maana nyie wote mmetoka kwenye maeneo yaliyopimwa? Unafiki huu hata siuelewi. Maeneo hayo ya Kipunguni na Kitunda hayajapimwa na yalikuwa hayana watu kabisa, na hasa eneo la Kipunguni lilipangwa kwa ajili ya kupanua uwanja wa ndege. Sasa watu wanaohamia kutoka nje ya Dar hasa wa kutoka Musoma wengi wao walikuwa wanashuka kwenye treni Pugu na kujikatia kijisehemu. Mwaka 1997, kulikuwa na nyumba chache tu, tena nyingi zilizojengwa kwa udongo na kuezekwa makuti, biashara ya kuku na mayai imebadilisha eneo lote, na watu kuzidi kufuata ndugu zao waliojiestablish hapo kumeongeza idadi ya watu. Vile vile kuna wengine wana shida ya mahali pa kukaa kwa uhaba wa vyumba na ukubwa wa kodi, visenti vyake amedunduliza anaenda kununua huko huko hakujapimwa. Hivi ni lini lakini watu watakaa na kupanga wao wenyewe, kuwa hapa tuwe na mtaa ulioonyoka na tupange mtaa wetu uelekeew wapi na kila mtu aache mita 3 kwa ajili ya njia ya kupita? Hata nyie mnapiga kelele humu hamuwezi kukubali, watu hipiga fensi eneo lote bila hata kubakisha uchochoro anasahau kuwa huko alikopita watu wamebakisha uchochoro ili apite. Hebu na tuache kulaumu serikali kwani eneo hilo lingepimwa hata hao waliojenga hapo wasingejenga, hata kama walikuwa na viwanja sie sie tungeenda kuloby kuchukua viwanja vyao, bora hivyo havijapimwa imekuwa salama kwao wamepata mahali pa kuishi, kwani Tanzania kila mtu ni mbinafsi na fisadi kwa namna moja au nyingine! Squater ziko kila mahali ila siku hizi badala ya kuvunja mipango miji inahalalisha umiliki wa nyumba na kuwasadia wao wenyewe kujipangia sehemu zao na kupata mitaa au njia. Kuna sehemu zoezi limekamilika na sehemu bado! Ila kama unakerwa na sqauter unaenda kutafuta nini huko? Si ukanunue kiwanja kwa matajiri wenzio cha mamilioni, tuachie wenyewe makazi yetu!


Tarehe December 07, 2008 1:21 PM, Mtoa Maoni: Mdau
Mtoa mada mbona Kibera hujaitaja. Kibera ambayo iko jijini Nairobi ni mbaya kuliko hapo


Tarehe December 07, 2008 3:01 PM, Mtoa Maoni: Anonymous
Mie nachokiona hapa hata kama hivi viwanja vimepimwa inawezekana ni style ya kuvipima kwani kama ninavyoelewa unaweza kwenda sehemeu ukakuta mtu amenunua sehemu kubwa au wanaita low density basi anajenda kisehemu kidogo kati ya eneo alilopewa basi baada ya muda maisha yanakuwa magumu anaamua kuuza kisehemu cha ardhi yake kwa mtu ambaye yeye kidogo anauwezo baada ya muda yule mwenye uwezo kidogo anaamua kununua na kwa jirani kule kunakuwa hakujajengwa basi anapitiliza kipimo na kujenga na sehemu ya uchochoro ambao hata haukuwa umepangwa kwa ajiri yake.Basi imagine kama watu watano wamefanya kama yeye mwisho ndio matokeo yake ni kama haya!!! kila kitu kimeharibika.


Tarehe December 07, 2008 4:31 PM, Mtoa Maoni: Mbwegelembwegele
ACHENI KUTETEA UJINGA . MIPANGO MIJI NI MUHIMU . MAKAZI SEHEMU ZILIZOJENGWA NA WAKOLONI ZIMEPANGWA VIZURI. MAKAZI MENGI SIKU HIZI HAYANA SEWAGE SYSTEM ,UNATETEA VIPI HILO .


Tarehe December 07, 2008 4:33 PM, Mtoa Maoni: Anonymous
WATANZANIA TUNAJIVUNIA SAANA KUISHI KTK NYUMBA ZA MAKUTI, KWA SABABU JIRANI ZETU WANAISHI KTK MTI . NI SEHEMU YA UMASKINI WA AKILI,HIVYO TUTAENDELEA KUWA MASIKINI KIMAISHA .


Tarehe December 07, 2008 5:11 PM, Mtoa Maoni: MBWEGELEMBWEGELE
KWA NYONGEZA TU , serikali lazima ilaumiwe. Umeshawahi kushuhudia kikosi cha zima moto kikishindwa kufikia nyumba yenye janga kwa sababu ya ujenzi holela ??


Tarehe December 07, 2008 8:19 PM, Mtoa Maoni: Anonymous
Kariakoo, Manzese, Magomeni, Mwananyamala na envirns zote za Dar zimekua hivyo hivyo. Acha kudhalilisha watu wa Musoma! Kwani ndio tu waliojazana kwenye envions za Dar zenye madhali kama hayo Michu anayoonyesha?


Tarehe December 07, 2008 8:40 PM, Mtoa Maoni: ROGERSBIZ
Kama huu ujenzi wa kiholela unaendelea, basi kutakuja tokea patashika bomoa bomoa itapokuja. Hizo nyumba lazima zivunjwe. we can't continue to do things like that if we are to move forward.


Tarehe December 08, 2008 2:05 PM, Mtoa Maoni: Anonymous
Jamani mie si walaumu wajenzi, tatizo liko kwenye hawa wapangaji wa miji kwani kabla ya kugawa viwanja inabidi kuwapo na mitaa(barabara) zinazo elekea barabara kuu kisha mabomba ya maji safi na maji machafu kwa kila kiwanja na baadae kila kiwanja 'frontage'lazima iwe umbali kadhaa kutoka barabarani na mwisho wapanga miji kwenda site kufuatilia huo mpangilio...kwa kufanya hivyo tutaepusha takakata hiyo hapo juu..


Tarehe December 08, 2008 2:32 PM, Mtoa Maoni: Anonymous
Umewataja maofisa woote waliopo hapo ila umemsahau mmoja MSTAHIKI MEYA pia yupo hapo, na anaona pia hayo yanayoendelea. Saasa, jifanye unaleta mipango miji yako na umemsahau Mh, mstahiki meya kupanga posho yake, weee, utakoma kuringa. Maana atakutukana kama mtoto mchanga na maneno machafu makali makali huku povu likimtoka kando ya midomo. hivyo nduzanguni tusiwalaumu sana watu wa mipango miji, suala ni hao madiwani chini ya mh. mstahiki meya ambaye ndiye kiongozi wao wanakwamisha sana maendeleo bongo watu hao. Sio siri.
Kama twataka kuwakumbatia viumbe hawa, basi, japo diwani awe na elimu si chini ya kidato cha sita, tena iwe kidato cha sita amefaulu sio alihudhuria shule, vinginevyo hadithi itakuwa ile ile. Natoa changamoto kwa wadau wote, ni manispaa ngapi, na miji mingapi ina madiwani waliohitimu kidato japo cha nne kwa asilimia 50 (50% ya madiwani walio ndani ya mchakato huo kwa manispaa husika au mji). Wengi huwa ni STD VII, sina maana hiyo elimu haina maana, bali je? kwa elimu hiyo watakuwa na upeo wa kuweza kurekebisha mipango miji yetu????? Afisa mipango miji ni mhitimu wa elimu ya chuo kikuu, bosi anayepitisha hizo ramani ndio huyo STD VII, tena alikuwa mtoro wa shule na kwa ujanja wake kaweza kuwashawishi watu wakamchagua, tena wengine wamechaguliwa ili hali tu ni wakereketwa wa chama fulani na wametoa pesa basi tena. Unatarajia nini hapo. Bado nasisitiza, kama kweli tupo siriaz, diwani awe mtu alokwenda shule. Hapo tutaendelea, ila hao waliopo kwa sasa ka tutaendelea kuwakumbatia, nasema maafisa wote sio wa mipango miji tu tutawalaumu bure.
MBxc


Tarehe December 08, 2008 3:33 PM, Mtoa Maoni: Anonymous
mada ni mzuri sana hata kama watu wa mipango miji wangekuwepo hadi serekali ya kijiji tatizo tumewaachia wanasiasa wakaamuwa nchi hii iwe ilivyo.inasikitisha kuona kuwa hata viongozi wa juu kabsa watashindwa kutofautisha kati ya afisa mipango miji,msanifu majengo, mhandisi na mkandarasi hizi ni fani ambazo zinategemeana na kufanya kazi kwa karibu sana inasikitisha katika halmashauri za miji yetu utakuta afisa mipango na mhandisi tu,Uzuri/beauty ya mji (majengo si kazi ya afisa mipango miji ni kazi ya msanifu majengo. mtaalamu wa mipango miji huweka tu mpangilio wa barabara na viwanja kwa mahitaji mbalimbali viwanda ,makanisa, misikiti,makazi ya watu,viwanja vya michezo.n.k
Undani /detail design hufanywa na msanifu majengo na mhandisi WATAALAM hawa ni wachache sana na hata wachache waliopo serikali yetu imeshindwa kuwatumia VEMA,Tanzania kuna (wasanifu majengo)architect takiribani 250 (waliosajili na bodi husika) inasikitika kusema kuwa katika mifumo ya serikali Tanzania nzima walioajiriwa ni pungufu ya 50.
je tutakuwaje na miji iliyopendeza kama ya wenzetu? je kama ramani master plan ya mkoloni ya kariakoo ya miaka hiyo ndiyo bado inaendelezwa tutapataje mji mzuri?KWANINI ISIFANYIWE MAREKEBISHO KUENDANA NA MAHITAJI YA SASA MIAKA YA 60/70 KARIAKOO ILIKUWA MAKAZI YA WATU(RESIDENTIAL PLOTS) LEO NI BIASHARA (COMMERCIAL PLOTS) MWONA HATUJABADILI SERA ZA KUENDELEZA MAENEO HAYA ? watanzania tuamke? tumia wataalamu husika
MSANIFU MAJENGO


Tarehe December 08, 2008 3:34 PM, Mtoa Maoni: Anonymous
Jamani hayo mahela yanayoliwa na serikali wangekuwa na akili wangekuwa wanapitia maeneo ya watu waliojenga kiholela na kujua ni idadi yao. Baada ya hapo wachague eneo ambalo limepimwa wajenge nyumba na kuwahamisha hao watu kwa makubaliano, lakini sio kuwavunjia nyumba halafu uwaambie watajijua watakakokwenda hiyo haipendezi na sio ubinaadamu hata kidogo, pesa ukiwalipa haitoshi mtu kujenga kama nyumba aliyokuwa nayo mwanzo. Kwa hiyo viongozi wetu sijui kama wanafikiria utu wa watu wengine.


Tarehe December 08, 2008 9:26 PM, Mtoa Maoni: Anonymous
Tukisemwa wabishi kwa kitu gani bwana? mtu atuseme lakini aangalie na kasoro zake nzito alizo nazo.Hawa wanatusema sisi wa TZ ni washamba, Hivi unakubaliana na hiyo kweli kwamba wa TZ ni washamba? Wao huangalia kaeneo kama hako kadogo ka mpango wa nyumba na kulinganisha na pia na kaeneo kadogo ka nyumba nzuri huko kwao Kenya na kusema jamani TZ ni bado wako nyuma sana.Naungana na mtoa maoni mmoja amesema labda kwa ambaye hajaenda Kenya akishikilia kujisifia kwao utaamini kuwa sisi ni washamba. Sisi kwa taarifa yako siyo washamba. Washamba ni wao.Umeenda sehemu inaitwa KIBERA. hata TZ tuna maeneo mabaya lakini ndugu yangu huwezi ukalinganisha na KEnya rafiki yangu.Kenya yale maji yaliyosuuzika ya kutoka chooni huko kibera ndiyo wanayokunywa wanadamu.Na hao ni watu weeeeengi wanaoishi kwashida hiyo na wamezoea hawana jinsi watafanya nini.Watu wachache wameshajinufaisha ndiyo wanafaidi jasho la wengi.Wachumaji juani ni wengi, na walaji kivulini ni wachache.Nyie achane tu wanaolaani ujamaa ujamaa, Ukweli ujamaa wa MWALIMU ulileta haki kwa Mtanzania na usawa pia.UMOJA, haki, na usawa. Kenya hakuna hiyo.Kwa taifa changa kama letu Ujamaa ilikuwa ni solution ya kuazia maendeleo yetu. Ndiyo maana pamoja na matatizo madogomadogo tuliyonaya sasa lakini misingi ile iliyowekwa na ujamaa ambayo ni UTU, USAWA, ubinadamu ,uzalendo, upendo imetusaidia sana kuwa na UMOJA na undugu.Hata tunapopotoka kidogo tu, kila mwananchi anayojuwa hiyo misingi, akiinama chini, akiinuka anasema eeh kweli jamani nimeteleza.Kwasababu dhamira inamsuta mwenyewe na anajirekebishwa na kurekebishwa vilevile, ni kama amevunja amri fulani ya msingi wa nchi. Lakini mwezetu KENYA yeye hiyo hajuwi, hata unapomweleza jamani jirani utu bwana, au ubinadamu bwana, utaona anakuangalia kwa jicho baya kana kwamba umemtukana hakuelewi kabisaa.Atakuuliza utu ninini, ubinadamu ninin, usiniletee mambo ya TZ hapa.Kwa hiyo ndugu hawa watani wetu hakuna chochote kile cha kutuambia, kama ni kazi wewe huwezi kufanya kazi au kuleta maendeleo mpaka Mkenya aje akwambie maendeleo bwana wewe hujaendelea. Acha bwana usijiweke nyuma kama koti wewe unanafasi kubwa ya kumwelimisha yeye, mimi hakuna chochote nitajifunza kutoka Kenya hakuna. sanasana Ukabila tu ambao si utaki, lakini nyumba, na mazingira mkenya asithubutu kutudharau kwa hilo.
Ahsante.


Tarehe December 09, 2008 7:32 AM, Mtoa Maoni: Patrick
Kwa taarifa yenu. Kwa mujibu wa UN HABITAT jiji la DSM ni asilimia 25 tu ndiyo iliyo surveyed. Ni kweli serikali na viongozi wapo, tena walikuwepo tangu enzi za mwaka 1961, wakati maeneo ya Buguruni na Manzese yalikuwa ni vitongoji na vichochoroni tu. Lakini kutokana na ongezeko la watu na vipato vyao wameweza kujenga wakati uwezo wa serikali hauko sambamba na mahitaji ya wajenzi. Njia pekee inayoweza kufuatwa ni 1. Ama maeneo hayo akabidhiwe developer kwa makubaliano ambayo wakazi wa makazi hayo hawataathirka na eneo hilo lipimwe na nyumba zijengwe kwa kuzingati vigezo vya beauty na huduma muhimu au 2.Serikali iwalipe fidia hao watu na kuwapeleka maeneo mengine. Hilini gumu mno na serikali haina ubavu wala fedha ya kufanya hivyo au 3 Mother nature ama kwa njia ya moto nyumba zote hizo ziungue na ziteketee kabisa halafu itakuwa rahisi kupima viwanja. La sivyo mtanedelea kuilaumu bure serikali. Hata hivyo kwa kuzingatia hayo kuna mpango wa CIUP--Community Infrastructural Upgrading Programe ambayo inalenga angalau kuweka ahueni kwenye maeneo hayo. Barabara na mitaro mnayoiona kutoka Mnyamani hadi Vinguguti; Manzese midizini, Tandale, Buguruni kwa Mandege ni matunda ya CIUP. Hiyo ndiyo habari yenyewe.

(source: michuzi blog, 06/12/2008)