Tuesday, 23 December 2008

Matokeo ya la Saba 2008

Matokeo la saba yatoka
Asilimia 80.73 ya watahiniwa wote waliofanya mtihani wa kuhitimu elimu ya msingi mwaka huu, wamechaguliwa kujiunga na shule za sekondari za Serikali nchini.

Akitangaza matokeo hayo leo asubuhi, Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Prof. Jumanne Maghembe amesema, kati ya wanafunzi hao waliochaguliwa, wasichana ni 188,460 sawa na asilimia 82.13 ya wasichana wote walifanya mtihani huo wakati wavulana waliochaguliwa kuingia kidato cha kwanza ni 244,800 ambao ni sawa na asilimia 76.66 ya waliotahiniwa.

Amesema idadi ya kufaulu kwa mwaka huu imeongezeka kwa asilimia 31.47 ikilinganishwa na ile ya mwaka jana.

Waziri Maghembe ameongeza kuwa, wanafunzi wengi wamefanya vizurii katika somo la Kiwashili ambalo wamefaulu kwa asilimia 73.41.

Somo lingine walilong`ara ni Sayansi ambapo wamefaulu kwa asilimia 68.24 na Maarifa kwa asilimia 61.03.

Ameitaja mikoa iliyoongopza kwa kufaulu nchini kuwa ni Dar es Salaam uliofaulu kwa asilimia 73.9, ukifuatiwa na Arusha kwa asilimia 66.2, Iringa kwa asilimia 64.1 na Kagera kwa asilimia 63.5.

Kwa mujibu wa Prof. Magembe, mikoa iliyoburuza mkia katika matokeo hayo ni Shinyanga uliofaulu kwa asilimia 34, Lindi asilimia 40, Mara kwa asilimia 42.6 na Tabora kwa asilimia 43.2.

(SOURCE: Alasiri, 2008-12-22 19:15:33 Na Sharon Sauwa, Jijini)

No comments: