Tuesday, 23 December 2008

Matokeo std VII: Tathmini yangu

Natofautiana na takwimu au maelezo yaliyotolewa na gazeti Alasiri, kwani zimepotosha picha halisi ya matokeo ya jumla.
Hapa ninanukuu aya kutoka gazeti Alasiri ambapo naona kuna dosari,
'Asilimia 80.73 ya watahiniwa wote waliofanya mtihani wa kuhitimu elimu ya msingi mwaka huu, wamechaguliwa kujiunga na shule za sekondari za Serikali nchini.'

Tathmini yangu (kulingana na mahesabu ya haraka haraka):

Watahiniwa wote jumla: 1,017,969

Waliofaulu mtihani jumla: 536,672 (=52.72% ya watahiniwa wote)

Waliochaguliwa kwenda sekondari za serikali jumla 433,260:
waliochaguliwa wasichana: 188,460 (=43.50% ya waliofaulu)
waliochaguliwa wavulana: 244,800 (=56.50% ya waliofaulu)
Jumla: 433,260 (hii ni sawa na 80.73% ya waliofaulu mtihani (536,672))

80.73% ya waliofaulu mtihani (536,672) ndio wamechaguliwa kujiunga na sekondari za serikali! Kwa hiyo, wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na sekondari za serikali (433,260) ni sawa na 42.56% ya wanafunzi wote (1,017,969) waliofanya mtihani wa darasa la saba mwaka huu!!!

Na waliofaulu mtihani ni sawa na 52.72% ya watahiniwa wote.

Wanafunzi ambao wamefaulu lakini hawakuchaguliwa kujiunga na serikali za serikali ni 103,412 sawa na 19.27%

Walioshindwa mtihani jumla yao ni 481,193 (sawa na 47.27% ya watahiniwa wote). Kati yao wasichana ni 274,283 (sawa na 57.0% ya walioshindwa wote) na wavulana ni 206,910 (sawa na 43.0% ya walioshindwa wote)

NB
Tathmini hii inatokana na takwimu kutoka Alasiri na Nipashe hapo chini. Kama kuna mapungufu yoyote ktk mahesabu au ukokotoaji, hilo ni kosa langu binafsi ktk kutafsiri tarakimu.

No comments: