Friday 9 May 2008

Manufaa ya ziara za Rais Kikwete nje

(SOURCE: Nipashe, 09 May 2008. By Mashaka Mgeta)
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Bw. Salva Rweyemamu, ametetea uamuzi wa Rais Jakaya Kikwete, kufanya ziara za kikazi nje ya nchi, licha ya kuwepo malalamiko yanayohusu wingi wa safari hizo.

Bw. Rweyemamu, alisema ziara za Rais Kikwete zinafanyika ikiwa ni utekelezaji wa majukumu yake, na hivyo kuleta mafanikio katika nyanja za uchumi na maendeleo.
``Rais ndiye Msimamizi Mkuu wa sera za ndani na nje ya nchi, hivyo sehemu zote mbili zinahusiana moja kwa moja na usimamizi na utekelezaji wake,`` alisema.

Alisema kwa mujibu wa Katiba, Rais hana vigezo vinavyoainisha idadi ya safari anazopaswa kuzifanya ndani na nje ya nchi. Pia kuchaguliwa kwa Rais Kikwete kuwa Kiongozi Mkuu wa Umoja wa Afrika, kunampa fursa zaidi ya kusafiri, kwa ajili ya kushughulikia masuala ya kitaifa na nchi nyingine barani humo.

Akizungumzia mafanikio ya ziara hizo, alitoa mfano ziara ya hivi karibuni iliyofanywa na Rais Kikwete nchini China, ilifanikisha Taifa hilo:
-kuisaidia Tanzania katika nyanja mbalimbali,
-kufuta deni la Dola milioni 315 za Marekani.
-kuahidi kusaidia uanzishwaji maeneo makubwa ya maendeleo ya kiuchumi na kutoa Yuan milioni 80,
-kutoa Yuan milioni 20 (fedha za nchi hiyo) kwa ajili ya ujenzi wa kituo cha kisasa cha mikutano cha Julius Nyerere na shughuli za maendeleo Zanzibar.
-kuanzisha ushirikiano wa masuala ya anga na safari za ndege kati yake na Tanzania,
-kufuta deni la Dola 500*** za Marekani za reli ya TAZARA na
-kujenga shule za kisasa za mfano za msingi na sekondari.

Alisema mafanikio ya ziara za Rais Kikwete, yalianza kupatikana tangu alipoingia madarakani, ingawa hali hiyo haitoi tafsiri ya kushindana kimaendeleo na mtangulizi wake, Rais wa awamu ya tatu, Bw. Benjamin Mkapa.
....................

***Dola 500 au Dola milioni 500?

No comments: