Monday, 16 November 2009

Ya kweli hayo?

........................................................................
........................................................................
Juzi nilipanda daladala moja kwenda mjini Tukuyu. Hiki kpanya kiko nyang'anyang'a. Bodi linatikisika na kupiga kelele gari iwapo kwenye mwendo, sakafu imetobokatoboka na baadhi ya vioo havifunguki kabisa. Kwa haraka haraka niliifananisha na torori bovu!

Ndani ya kioo cha dereva kulikuwa na 'stika' 2.

Stika ya kwanza imeandikwa 'Manchester United FC' na nembo ya MU.

Stika ya pili ilikuwa na maandishi 'This Car is Protected by the Blood of Jesus'.
........................................................................
........................................................................

No comments: