Friday 11 January 2008

Pongezi za ubalozi

MAONI YA BALOZI WA UINGEREZA, PHILIP PARHAM, JUU YA MAAMUZI YALIYOCHUKULIWA NA SERIKALI KUHUSU REPOTI YA UCHUNGUZI BENKI KUU

“Mara nyingi nimekuwa nikisema jinsi ilivyo muhimu kwa serikali kuonekana ikishughulikia kikamilifu tuhuma nzito za rushwa.




Hivyo nimefurahi kusikia kwamba ukaguzi maalum uliofanywa kwenye akaunti ya "External Payment Arrears" (EPA) Benki Kuu sasa umekamilika, na kwamba Rais Jakaya Kikwete amefanyia kazi kwa haraka kabisa yaliyogunduliwa. Tunampongeza Rais Kikwete kwa maamuzi aliyochukua.
Ni sahihi kabisa kwamba hatua za kinidhamu zinapaswa kuchukuliwa dhidi ya wale waliohusika na ulipaji wa fedha hizo kwa njia zisizo halali, na vilevile dhidi ya wale walioshindwa kuchukua hatua pale ambapo ishara za "mambo kutokwenda sawa" zilipojitokeza kwa mara ya kwanza.

Pia itakuwa muhimu kama uchunguzi ulioanzishwa na Rais utafanyika kwa haraka na kikamilifu. Ni vigumu kuamini kama ufisadi wa uzito na kiwango hiki unaweza kuhusisha Benki Kuu yoyote.
Wale wote waliohusika, na waliojinufaisha kwa fedha zilizoibiwa, lazima wawajibishwe. Kufanya hivyo ni muhimu sio tu kujenga imani kwa Washirika wa Maendeleo, bali pia imani kwa Watanzania na wawekezaji wa nje, ambao ustawi wa Watanzania unategemea.

Tunasubiri kusikia zaidi juu ya ukaguzi uliofanyika, na pia hatua ambazo serikali itachukua katika kuyafanyia kazi mapendekezo yaliyotolewa.
Vilevile tunasubiri matokeo ya uchunguzi ambao Rais ameuanzisha, na tunatumaini tuhuma nyingine nzito za rushwa nazo pia zitashughulikiwa kikamilifu.”



John Bradshaw
Press Officer
British High Commission
Mobile: +255 (0)754 764276
Email: john.bradshaw@fco.gov.uk

No comments: