Tuesday 29 January 2008

Ndiye mama ntilie, machinga na tajiri mkubwa!

Napenda kuongelea jinsi wenzetu walivyofunguka macho kimaisha hapa duniani hasa ktk nchi zilizo ktk mabara ya Marekani na Ulaya! Hizi nchi kwa kweli zimeendelea na si kiteknolojia peke yake bali pia kiupeo wa mawazo.
Nyumbani kwetu tuko na umaskini wa kiuchumi kwa walio wengi. Lakini kifikra sisi ni matajiri, na kinyenzo pia hatuko nyuma. Tuna utajiri wa ardhi na maliasili nzuri ambayo haijahariwa kimazingira. Tuna idadi kubwa ya watu, watu pia ni muhimu ktk gurudumu la maendeleo! Ndio maana wenzetu wa nchi za magharibi hukaribisha wageni na pia kuhamasisha uzazi mwingi kwa wakazi wake ili kuhakikisha idadi ya watu inaongezeka au inabaki ile ile isje kupungua mbeleni. Watu ni muhimu, na sisi huko nyumbani hatuna umaskini wa vizazi na watu. Kwa maana hiyo tuko tayari kabisa kulianzisha gurudu la maendeleo. Kwa bahati mbaya tunakawia kuliazishia safari hilo gurudumu!!!

No comments: