Friday 17 August 2007

Maandamano ya CHADEMA

Soo la Zito:Tibaigana sasa ahaha
17 Aug 2007By Emmanuel Lengwa, Jijini
Lile sakata la Mbunge machachari wa Chadema aliyesimamishwa na Bunge juzi juzi, Mheshimiwa Zitto Zuberi Kabwe limemchanganya Kamishna wa Polisi wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, mzee mzima, Alfred Tibaigana. Mkanganyiko huo unatokana na barua tatu tofauti ambazo Kamishna Tibaigana amelimwa na chama cha Chadema zote zikiomba kibali kwa ajili ya kufanya maandamano kesho Jijini. Kwa kauli yake mwenyewe, Kamishna Tibaigana ameliambia gazeti hili leo asubuhi kuwa mambo ya akina Zitto yamemchanganya akili kwa sababu ametumiwa mibarua mitatu tofauti na sasa hajui awaelewe vipi.
Chama hicho kimepanga kufanya maandamano kesho ambayo yatahitimishwa kwa mkutano wa hadhara pale kwenye viwanja vya Jangwani, ambapo Mbunge huyo machachari aliyesimamishwa kuhudhuria shughuli za bunge hadi Januari, Bw. Zitto Kabwe atauelezea umma kilichomsibu Bungeni.
``Barua zote hizo kila moja inataja sehemu tofauti ambayo maandamano yataanzia, huku zikiwa zimesainiwa na mtu mmoja…sasa mimi siwaelewi,`` amesema Kamishna Tibaigana. Amesema moja ya barua hizo inasema maandamano yataanzia Mnazi Mmoja, nyingine inasema yataanzia Ubungo na nyingine haisemi mahali yatakapoanzia,`` akafafanua.
Kufuatia kujikanganya huko, Kamishna Tibaigana amesema amemuandikia barua mtu aliyesaini barua hizo ili aende ofisini kwake wajadiliane kabla ya kutoa uamuzi wa kuwapa kibali hicho.
``Nimemuita Bw. Erasto Tumbo ambaye amesaini barua hizo zote kwa niaba ya Katibu Mkuu aje ofisini…akija tutajadiliana na ndio nita-react kwao,`` akasema Kamishna Tibaigana. Maandamano hayo yaliyopangwa na CHADEMA, yanaungwa mkono na vyama vingine vitatu vya upinzani vya NCCR Mageuzi, TLP na CUF.

Kwenye kilele cha maandamano hayo, Mhe. Kabwe ambaye sasa anaitwa shujaa, anatarajiwa kuhutubia wananchi na kumwaga hadharani mambo yote yaliyopelekea kupigwa `stop` kujihusisha na shughuli za Bunge.

Pia Katibu Mkuu wa chama cha wananchi, CUF, Maalim Seif Sharif Hamad anajipanga `kumwaga` siri kibao kuhusu mazungumzo ya muafaka wa Zanzibar yaliyokuwa yakiendelea baina yake na Katibu Mkuu wa , CCM, Luteni Mstaafu Yusufu Makamba. Maandamano hayo yamepangwa kuanza kesho saa 4:00 asubuhi, na kuhitimishwa kwa mkutano wa hadhara utakaoanza saa 6:00 mchana kwenye viwanja vya Jangwani.
* SOURCE: Alasiri

Bado sijapata yale majadiliano ya Bungeni juu ya hoja ya mhe. Zitto. Na hii adhabu ya miezi minne (4) wameifikiaje; ni kwa nini iwe ya miezi 4 na sio mwezi mmoja au miwili?
Hili tukio la kusimamishwa Mhe. Zitto linanikumbusha yaliyomkuta mhe. George Galloway MB wa Bethnal Green, London wa chama cha RESPECT, ambaye naye alisimamishwa kazi (House of Commons) kwa siku 18.


George Galloway response to 18 days suspension, 17/07/2007
"Once more and yet again I have been cleared of taking a single penny or in any way personally benefiting from the former Iraqi regime through the Oil for Food programme or any other means. The Commissioner's report states that unequivocally no less than six times. The Commissioner further states that it would be a "travesty" to describe me as a "paid mouth-piece" and that my actions on Iraq stemmed from "deep conviction." This is therefore an argument about the funding of a political campaign to lift non-military sanctions on Iraq, which killed one million people, and to stop the rush to a war which has cost the lives of hundreds of thousands more. The Committee appear utterly oblivious to the grotesque irony of a pro-sanctions and pro-war Committee of a pro-sanctions and pro-war Parliament passing judgment on the work of their opponents, especially in the light of the bloody march of events in Iraq since this inquiry began four years ago. They describe that as questioning their integrity and bringing Parliament into disrepute. The House would do well to honestly calibrate exactly how its reputation on all matters concerning the war in Iraq stands with the public before deciding who precisely has brought it into disrepute. After a four year inquiry - costing a fortune in public funds - the report asks me to apologise for not registering consistently the Mariam Appeal I established (the Commissioner concedes that I did so, but randomly) and for using House of Commons resources allocated to me to campaign against the policies of those now sitting in judgment on me. The Committee of MPs acknowledges that "had these been the only matters before us, we would have confined ourselves to seeking an apology to the House." However, in a surprisingly thin-skinned rejoinder, the MPs complain that because I questioned their impartiality and made trenchant criticisms of evidence and witnesses (which, incidentally, they don’t attempt to refute in most cases) I am to be suspended for 18 days. I reiterate that the Commissioner is right to state that he found no evidence that I benefited personally in any way from any Iraqi monies and moreover I never asked any of the Mariam Appeal's donors - the King of Saudi Arabia, the Emir of UAE, or Fawaz Zureikat, the chairman of the Appeal - from where they earned the wealth from which they made donations to a campaign to end sanctions and war." George Galloway MP

source: http://www.georgegalloway.com/

No comments: