Tuesday, 19 January 2010

Mmemwona JK kazini jana?

Jana nilifurahishwa sana na uamuzi wa Rais wetu Ndugu Jakaya Mrisho Kikwete wa kukataa kukabidhi gari la wagonjwa kwa wasiohusika.

Hii inaonyesha umakini wake ktk utendaji na ufuatiliaji wa mambo kwa karibu (up to 'minute' details!!).

Mwaka jana ktk moja ya ziara zake mikoani, Rais JK aliahidi kusaidia gari la wagonjwa kwa zahanati ya wanakijiji (kijiji fulani) kule Longido. Lakini watendaji kule Ngorongoro wakamtuma mkurugenzi wa Loliondo kulichukua gari ikulu! Sijui hii ilikuwa ni bahati mbaya au ndio ile janja janja yetu ya ki-TZ!!!!!!
(Note: Haya (Longido na Loliondo) ni maeneo mawili tofauti kiutendaji!!)

Baada ya maongezi mafupi, Rais akamwelemisha huyo mkurugenzi kuwa wahusika ndio wanatakiwa kuja kupokea hilo gari ikulu na si vinginevyo!

Na kauli ya mwisho ya Rais kwa huyo director wa Loliondo ilikuwa "Hatukupi (gari)" na Rais akaondoka moja kwa moja kuelekea ikulu!!!

Saaafi sana mheshimiwa JK!!! Unafaa!

Good news: Wa Mbozi wao walipokea gari lao kupitia kwa Mkurugenzi wetu L Chillewo. Gari hiyo ni kwa ajili ya zahanati kule maeneo ya Kamsamba!

No comments: