Wednesday, 20 January 2010

CAN vs. Premier League

Ujio wa mashindano ya kombe la mataifa huru ya Afrika wiki iliyopita umeleta kuleta mwingiliano wa utazamaji wa mechi siku za mwisho wa juma.

Jumamos iliyopita watazamaji tulilazimishwa kulipia na kutazama mechi 1 na nusu. Mechi ya Manchester United v. Burnley ilianza saa 12.00 jioni za Afrika Mashariki na wakati huo huo mechi ya Nigeria v. ....? ikawa inaanza saa 1.00 za usiku.

Mwenye TV yake yenye channel za DSTV (Super Sports) akaeleza kuwa Mechi ya Man Utd V. Burnley sh. 200/= (kipindi cha 1 tu!) na mechi yote ya Nigeria sh.200/= jumla 400/=. Na kweli mechi hiyo ya Man Utd ilionyeshwa kipindi cha kwanza tu! Ilibidi nilipie 200/= ili niangalie kipindi cha kwanza, kisha nikahamia nyumbani kusikiliza matangazo ya BBC FM ingawa magoli yote matatu sikuyaona kwenye TV (yalifungwa kipindi cha 2). Na mechi ya Nigeria niliiona nyumbani pia (TBC1)!

Yaani utaratibu ni kwamba mechi za Afrika zinachukua umuhimu wa kwanza, na usiombee mwenye TV awe shabiki wa Arsenal au Liverpool ama Chelsea, hata hicho kipindi kimoja cha Man United tusingeonyeshwa!! Maana waliokuwa ktk TV za shabiki wa Chelsea walionyeshwa mchezo wa Chelsea v. Sunderland wakati sisi tukiangalia wa Man Utd sehemu tofauti!

Lakini hizi mechi za Afrika zinaonyeshwa pia na TV ya Tanzania (TBC1) tena ni bure, sijui ni kwa nini mashabiki wasiangalie majumbani au ktk baa kwa kinywaji kimoja kama Pepsi au Coca-Cola kwa sh.500/= tu!!! Na kuna sehemu nyingine za biashara pale Dar mechi hizo huonyeshwa bure bila kiingilio au haja ya kununua kinywaji au chakula.

Sasa nasubiri Jumamosi ijayo nikaangalie kipindi cha kwanza mechi ya Man Utd v. Hull City!!

Anyway, "This Is Living" (and Other Stories), By Agoro Anduru!!

No comments: