Tuesday, 19 January 2010

Hongereni Star TV na Futuhiiiii!

Kuna kundi la vichekesho (comedy) ambalo linanifurahisha sana. Kila alhamis saa 3 hadi 4 usiku kupitia Star TV. Hawa sio wengine bali ni Futuhi. Babu Mkombe, Okechi, Chacha (Ntakobhoha Monto, Top!) na wenzao, wanafanya vizuri sana ndani ya Futuhi wakiwa ktk jiji la Mwanza!

Star TV nao wanafanya vizuri, hasa Mtangazaji Yvonne Joel anafanya kazi nzuri kiutangazaji. Nilifurahishwa sana kazi yake siku ya mazishi ya Mzee Rashid Kawawa -live coverage yake ilikuwa ya kiwango cha hali ya juu sana (naweza kusema kazi yake Yvonne Joel ni ya kiwango cha kimataifa kama vile CNN,Sky News, BBC n.k.)

No comments: