Friday, 11 July 2008

Uwanja wa Taifa au makumbusho ya Taifa?

Bado najiuliza na sipati jibu. Kwa kifupi mimi nina-argue kuhusu lengo la kuwa na kiwanja cha mpira nini?

1. Kiwanja ni sehemu mojawapo ya kutoa burudani kwa mashabiki wa mpira au tukio lolote linalofanyika uwanjani.

2. kiwanja ni kitega uchumi. Hakuna haja ya kujenga uwanja mkubwa na wa kisasa kama lengo sio kutafuta au kuongeza mapato kifedha.
Lakini wenye uwanja (serikali) wanaubania uwanja na hautumiki, na wanapoombwa na shirikisho la soka wanachukua muda mrefu sana kutoa ruhusa.
-hivi ulijemgwa kwa ajili ya nini hasa?
-hela zilizotuminka kuujenga zitarudi vipi endapo mageti yanafungwa karibu mwaka mzima. Unaweza kukuta kwa mwaka inafanyika mechi moja au mbili tu! Jamani hizo hela zilizoujenga si ni za wananchi na zinakatwa kila kurudisha deni (toka kwa wachina)? Mbona sekali haina uchungu wa kurudisha hizo hela?

Chukulia uzoefu wa uwanja wa Wembley Uingereza. wenye uwanja (chama cha soka, the FA) wamepania kurudisha deni la hela walizokopa kuujenga uwanja huo ifikapo mwaka 2012, na ikiwezekana wawe wameshaanza kuingiza faida kipindi hicho.

Nimeesha eleza sana juu ya mikakati yao ya kuingiza mapato zaidi kila mwaka (soma makala zangu za awali kuhusu Uwanja wa Taifa).

Achana na Wembley, chukulia uwanja wa timu ya mpira wa miguu ya Reading FC. Reading FC wameingia mkataba na timu ya mpira wa 'rugby' ya London Irish hadi mwaka 2025. Hao London Irish ni kama wapangaji -wanalipa pango kwa Reading FC. Timu zote hizo zinautumia uwanja kwa zamu -kwa hiyo hicho ni kitega uchumi cha ziada kwa timu ya Reading.

Huwa najiuliza sana kuhusu sisi watanzania kwa nini tuko nyuma sana kibiashara? Utadhani tuko matajiri sana.

Hata ktk utalii tuko nyuma, utashangaa watalii watua Nairobi ili wakauone mlima Kilimanjaro na Serengeti .....! (utajaza mwenyewe!)
..........................................................

Hiyo ni mara ya kwanza kwa serikali kuruhusu uwanja huo uliogharimu zaidi ya bilioni 50, kutumika katika michuano ya CECAFA hasa ngazi ya klabu, ambapo mwaka jana serikali iliikatalia CECAFA, kuutumia uwanja huo kwa ajili ya michuano ya Chalenji inayozishirikisha nchi za ukanda wa Afrika Mashariki na Kati.

1 comment:

MOSONGA RAPHAEL said...

Uwanja mpya ruksa Kagame

(SOURCE: Nipashe, 2008-07-11 08:54:00 By Jimmy Charles)


Serikali imeruhusu Uwanja Mpya wa Taifa wenye uwezo wa kuingiza watazamaji 60,000 utumike kwa ajili ya baadhi ya michezo ya kuwania Kombe la Kagame inayotarajia kuanza kesho,jijini Dar es Salaam na mkoani Morogoro.

Hatua hiyo ya serikali kuruhusu uwanja huo ambao bado unaelezwa uko kwenye matengenezo imekuja baada ya Baraza la Soka kwa nchi za Afrika Mashariki na Kati (CECAFA) kulitaka Shirikisho la Soka nchini (TFF), kwamba uwanja huo.

Akizungumza na waandishi wa habari jana, Rais wa CECAFA na TFF, Leodger Tenga, alisema kuwa wanaishukuru serikali kwa kukubali maombi yao ya kuutumia uwanja huo, ambapo CECAFA inaamini hatua hiyo itasaidia kuutangaza uwanja huo wa kisasa.

``Kwa kweli tunaishukuru sana serikali kupitia Wizara ya Habari, Utamaduni na Michezo kwa kuruhusu tuutumie uwanja mpya, ni hatua kubwa ambayo itasaidia katika kuutangaza uwanja huo kimataifa,``alisema Tenga.

Tenga, aliongeza kuwa mbali ya kuutangaza uwanja huo lakini pia utasaidia katika kuwavutia mashabiki wengi zaidi kujitokeza katika kushuhudia michezo itakayochezwa kwenye uwanja huo.

Alisema uendeshaji wa michuano hiyo unahitaji fedha nyingi, ambapo jumla ya fedha zinazohitajika ni milioni 200, hivyo kwa kupata nafasi ya kutumia uwanja huo kuna uwezekano ikasaidia kuongeza pato kupitia makusanyo ya milangoni.

Aidha, Tenga alisema pamoja na kuruhusiwa kuutumia uwanja huo lakini pia wamepewa masharti, ambapo michezo itakayochezwa hapo ni michezo miwili ya ufunguzi kati ya Simba na Tusker ya Kenya na Yanga na APR ya Rwanda.

Aliongeza kuwa wanaangalia uwezekano wa kuutumia uwanja huo kwa ajili ya michezo ya hatua ya robo fainali hadi fainali.

Hiyo ni mara ya kwanza kwa serikali kuruhusu uwanja huo uliogharimu zaidi ya bilioni 50, kutumika katika michuano ya CECAFA hasa ngazi ya klabu, ambapo mwaka jana serikali iliikatalia CECAFA, kuutumia uwanja huo kwa ajili ya michuano ya Chalenji inayozishirikisha nchi za ukanda wa Afrika Mashariki na Kati.