Binti mmoja wa umri wa miaka 16 (Berks) amepigwa stop kufanya mitihani ya 'gsce' (kidato cha 6?) kwa kujitoboa juu ya midomo yake na kujiwekea mapambo ya vyuma kama heleni. Sheria za shule haziruhusu mapambo kama hayo. Binti huyo alijiwekea urembo huo wakati wa likizo ya pasaka na akaambiwa na 'mtaalamu' wake kuwa asivitoe viheleni kwa wiki 5 mfululizo!
Sasa itabidi aamue; mtihani au urembo! Kazi kwake!!
Mambo haya hata Ulaya yanapigwa vita -yasichanganywe na elimu mashuleni, lakini huko kwetu watu ndio kwanza watoto wanaiga! Labda ni kwa vile hawaelewi kinachoendelea upande wa pili wa shilingi.
Tusiige kila kitu jamani!
Tuesday, 29 April 2008
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment