(source: jamboforum mail blitz)
MSIBA MKUBWA UINGEREZA
(Reading)
*Peter Gachuma,Thomson Msigwa
Wafariki Dunia..
-------------
Wanajumuiya wa UK tumepokea habari Ya kusikitisha za kifo cha Wenzetu Peter Gachuma na Thomson Msigwa kilichotokea leo huko Tanzania kwa ajali ya gari wakitokea Tarime (mara) kuelekea Mwanza.
Marehemu Peter Gashuma alikua akisoma university of Birmingham na kuishi Reading,vilevile Marehemu Thomson Msigwa alikua anaishi Reading Uingereza, Marehemu walikwenda nyumbani (Tanzania) wiki iliyopita kwa likizo fupi.Marehemu Thomson Msigwa ameacha mke na watoto.
*Mwenyezi mungu azilaze Roho za Marehemu Mahali pema peponi Amen.
----
**Tutaendelea kuwajulisha habari zaidi kadri zinavyotufikia..
Monday, 14 April 2008
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment