Monday, 21 April 2008

Mheshimiwa Rais

Kumekuwa na tetesi na pia tuhuma za wazi zinazowakabili wasaidizi wako. Watanzania wanasubiri hatua kutoka kwako za kuwawajibisha maana wanalichafua hata jina lako.

Unapoendelea kuwa kimya unatufanya tuanze kufikiria vingine juu yako.

Mimi naamini kabisa wewe Mheshimiwa Rais hauhusiki kwa namna yoyote ile na uozo huu, na ndio maana nakuomba uwaondoe hawa wanaorudisha nyuma juhudi zako ktk awamu ya 4 za 'Ari Mpya, Kasi Mpya na Nguvu Mpya'.

Usisahau 80% ya wananchi walikupa imani yao uwaongoze, ni vizuri ukiwasikiliza kilio chao ktk kipindi hiki. Ebu rudisha imani waliyoonyesha kwako, usiwakatishe tamaa.

No comments: