Tuesday, 1 April 2008

Mbona ajali zinazidi Temeke?

Nawaomba mamlaka ya leseni kuwa makini ktk kutoa leseni kwani inaoneka wengi wa madereva hawana kiwango kinachotakiwa cha kuendesha magari hasa ya kibishara.

....................................
....................................
Daladala laacha njia na kujeruhi watano
(* SOURCE: Alasiri, 01 Apr 2008)
By Mwandishi Wetu, Mbagala

Watu watano wamejeruhiwa baada ya daladala walilokuwa wakisafiria kuacha njia na kuyavaa mabomba kadhaa yaliyokuwa yameegeshwa kando ya makaburi ya Mbagala Mission Jijini.

Ajali hiyo imetokea mishale ya saa 2:25 leo asubuhi wakati daladala aina ya Toyota DCM, lenye namba za usajili T 677 ADJ, likitokea Mbagala Rangi Tatu kuelekea Mwenge lilipokumbwa na mkasa huo wa kuacha njia.

Hali hiyo iliwafanya abiria kumkwida dereva na kumtaka awarudishie nauli, kwani alionekana dhahiri kuwa alikuwa akiendesha kizembe, hasa baada ya njiani kuwahi kujibishana na trafiki aliyewasimamaisha katika barabara ya Kilwa na kumshauri ashushe abiria lakini akakaidi akidai kuwa gari lake halina matatizo.

Hata hivyo, dereva huyo aliokoka toka kwenye kipigo kikali cha abiria baada ya polisi kufika mahala hapo na kumuokoa.

No comments: