Tuesday, 29 April 2008

Ukweli na Haki

Mara nyingi ingetegemewa watu wakweli na watenda haki katika jamii wangekuwa wanapendwa na watu wote. Lakini kinyume chake watu hao wanaweza kukumbwa na wakati mgumu sana ktk maisha yao kwa ujumla. Hasahasa hawapendwi na wenye mamlaka, madaraka ya juu na watu walio ktk nafasi kama hizo!
Wanyonge wasio na nguvu na uwezo kimaisha ndio huwakumbatia na kuwatuza wasema kweli na watenda haki.
Kuna msemo, 'shujaa hathaminiwi nyumbani kwao'. Na watu wengine husema hata Yesu hakuthaminiwa na ndio maana aliteswa kwao!

No comments: