(SOURCE: Alasiri, 29 Apr 2008. By Mwanaidi Swedi, Temeke)
Watu wapatao kumi (majambazi) wakiwa na silaha, wamevamia nyumba moja Jijini Dar es Salaam na kukomba vitu mbalimbali pamoja na pesa taslimu shilingi milioni moja. Mali zilizoibwa ni pamoja na televisheni (1), deki (1) na simu za mkononi (2) aina ya Nokia.
Kamanda wa Mkoa wa Kipolisi wa Temeke, Emmanueli Kandihabi, amesema tukio hilo lilitokea jana majira ya saa 8:20 usiku huko Yombo Dovya.
Watu hao walivamia vyumba ya Bw. John Martine,43, na kuvunja mlango kwa kutumia jiwe kubwa almaarufu kama fatuma. Baada ya kuvamia nyumba hiyo, walimjeruhi mwenye nyumba kwa panga kabla hawajaanza kupora mali. Majeruhi alitibiwa katika hospitali ya Temeke na kuruhusiwa.
Kamanda amesema Polisi wanaendelea na uchunguzi ili kuwatia mbaroni watuhumiwa hao.
Tuesday, 29 April 2008
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment