Tuesday, 15 April 2008

Nukuu bora! (kwa kweli nimeipenda)

(Source: Majira, 15.04.2008 0146 EAT
Na Joseph Lugendo, Dodoma)
MBUNGE wa Maswa, Bw. John Shibuda (CCM) alitahadharisha kwamba dhana ya Watanzania kuwa na mali isigeuzwe mlango wa kuwahujumu wengine na kwamba kufanya hivyo kutakuwa sawa na kutengeneza kundi la wanyonyaji, ambalo lilikataliwa wakati wa ukoloni.
"Tuliwafukuza wanyonyaji si kwa rangi bali kwa tabia, hulka na silka yao na hivyo tuwe makini tusije tukawatengeneza wanyonyaji weusi," alisema.

No comments: