Leo nimeota ndoto.
Katika ndoto niko ktk msafara wa Baba wa Taifa, Mwalimu Nyerere kutembelea kambi ya Jeshi la Kujenga Taifa kule Tabora. Ilikuwa ni baada ya kupata uhuru kati ya 1961 na 1966.
Vijana walimpokea Mwalimu wa furaha na nyimbo kemkem za kuhimiza maendeleo na za ukombozi. Sauti za vijana zilikuwa zinavutia kama vile usiku wa 'karaoke'! Kila alikopita Mwalimu alipokewa kwa nyimbo za hamasa!
Ilikuwa ni furaha sana ktk mazingira yale niliyoyaona kambini, na Mwalimu alifurahi sana!
Ila sijui maana ya hii ndoto, na pia ktk miaka hiyo nilikuwa bado kuzaliwa. Ama ni kwa vile nilipitia kambi ya Tabora? Au labda ni kwa kuwa tumem'miss' sana Mwalimu ktk kipindi hiki ambacho ngalawa yetu inaelekea kuyumba na kujaa maji (maana ina matundu mengi)?
Saturday, 19 April 2008
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment