(kutoka: majira, 23.04.2008 0129 EAT. Na Rehema Mohamed )
Polisi kuvaa sare mpya
JESHI la Polisi nchini limezindua sare mpya za aina mbalimbali na alama za vyeo kwa askari wake zitakazovaliwa kulingana na mazingira ya kiutendaji hatua inayolenga kuboresha utendaji wake.
Kamishna wa Utawala na Fedha wa Jeshi hilo, Bw.Clodwig Mtweve, amesema sare hizo ni pamoja na zile zitakazovaliwa na maofisa wakuu katika tafrija maalum, kufanyia kazi na usafi kwa askari na maafisa wa ngazi zote.
Sare ya kwanza: 'tacron' ya kaki au 'jugle' ya kijani kwa wanaume, blauzi ya 'tacron' nyeupe na sketi ya nevi bluu kwa wanawake pamoja na kofia ya bereti ya brauni.
Nyingine ni suti ya khaki au 'jungle' ya kijani kwa wanaume na blauzi ya 'tacron', sketi ya nevi-bluu kwa wanawake pamoja na mkanda wa 'tacron' khaki au 'jungle' ya kijani kwa maofisa wanaume na kofia ya aina ya bereti nyeusi au nyekundu.
Sare nyingine ni shati nyepesi ya khaki aina 'jungle' ya kijani kwa wanaume na shati nyeupe kwa wanawake,suruali 'tacron' khaki au 'jungle' ya kijani kwa wanaume na sketi ya nevi- bluu kwa wanawake,kofia aina ya bereti nyeusi au nyekundu itakayovaliwa na askari na maofisa wa ngazi zote.
Nyingine ni kombati aina ya 'jungle' ya kijani na kofia aina ya bereti nyeusi au nyekundu itakayovaliwa wakati wa operesheni tu, pamoja na sare ya suti ya khaki na kofia ya khaki itakayovaliwa wakati wa kufanya usafi kwa maaskari wa ngazi zote.
Sare hizo zitaanza kuvaliwa kuanzia Mei mosi mwaka huu.
Wednesday, 23 April 2008
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment