Tuesday, 10 June 2008

Wanawake, ngono na kondomu!

Njia rahisi ni kwa mwanamke kujinunulia kondomu anazoona zinafaa (ki-ubora) na za kutosha (ki-idadi) ili zitumike pale anapojihusisha na tendo la ngono.
Pia, kwa kusema ukweli, mwanamke mwenyewe anao uwezo kabisa kuhakikisha kuwa kondomu inavaliwa na inatumika kama ataamua kufuatilia kabla ya tendo lenyewe maana mwanamke ndie kama kondakta wa 'bus'; abiria lazima alipe nauli kabla ya safari!!
-mosonga2002@yahoo.com
...................

(SOURCE: Nipashe, 2008-06-10 10:57:51 Na Kibuka Prudence, PST, Kagera)
Meneja wa Shirika la PSI mkoani Kagera Bw. Clement Mbogo, amesema wanawake wana uwezo wa kuhamasisha matumizi ya kondomu na amewashauri kujali maisha yao kwa kuacha kudharau umuhimu wa kutumia kondomu katika kupiga vita maambukuzo ya Ukimwi.

Alisema nafasi ya mwanamke katika kumshawishi mwanaume kutumia kondomu ndiyo njia pekee ya kupunguza kuenea kwa maambukizo ya virusi vya Ukimwi na magonjwa mengine yanayotokana na zinaa.

Alibainisha kuwa kumekuwepo na ushirikiano mdogo kutoka kwa mwanamke mara anapokuwa katika mazingira ya kukutana kimwili na mwanamme, hali ambayo inamfanya mwanamume kujiamulia kwa lo lote atakalo.

Alisema wanaume wengi wamekuwa wakitumia udhaifu wa wanawake wakati wanapokuwa sehemu za faragha na kuamua kutotumia kondomu huku wakiwalaghai wenzao wao kuwa wamezitumia wakati wanapokuwa katika mahusiano ya kimapenzi.

Hivyo, aliwataka wanawake kote nchini kutoona aibu wakati wanapokuwa na wapenzi wao wajitambue kuwa nao wanahaki ya kutoa ushauri wa matumizi ya kondomu ili kuokoa maisha yao na kuyaokoa maisha ya wenza wao.

No comments: