Monday, 2 June 2008

Bendera ya Taifa letu

Haya hapo chini ni maoni yangu mahala fulani kuhusu tafsiri ya rangi za bendera yetu ya Taifa hasa rangi 'nyeusi'.
Nikiangalia mfano wa wenzetu wa Afrika Kusini*, wao wamebainisha kabisa rangi; -nyeusi na nyeupe- kwa maana kuwa wapo weusi na wasiokuwa weusi ambao wanawakilishwa na rangi nyeupe*!

Ktk maoni yangu haya sina maana ya kuwabagua weupe ila ningependa kujua kama tafsiri ya rangi 'nyeusi' ktk bendera yetu inawawakilisha pia wenzetu wasiokuwa weusi. Ningependa nao wajisikie/waone kuwa wanawakilishwa ktk alama muhimu ya Taifa letu.

Wangwana, kama nimetoka nje ya mstari napenda kuomba radhi 'in advance', lakini nadhani sio vibaya/mwiko kuuliza -eti jamani!
Kuuliza si ujinga!
...........................
...........................
(Na Mosonga. Tarehe October 30, 2007 9:00 PM)
Jamani naomba tuandae mjadala wenye Kichwa cha habari:
Bendera yetu ya Taifa inakidhi matakwa ktk mazingira ya sasa?
Wakati wa kupigania uhuru, kujikomboa na kupata uhuru Tanganyika na mapinduzi ya Zanzibar, rangi za bendera yetu zilikuwa na tafsiri yake ktk mazingira ya wakati huo. Lakini sasa mazingira yamebadilika.
Rangi hizo ni:
Kijani- uoto wa asili
Njano-madini na utajiri
nyeusi-wananchi (kwa maana ni weusi??)
bluu-maji bahari, maziwa na mito

Swali langu liko ktk rangi nyeusi ktk mazingira ya leo inawakilisha nini?
Je ni wakati muafaka kubadili au kuongeza rangi ktk bendera ya taifa ili iwakilishe watanzania wa asili (race) tofauti na weusi??
Naomba nieleweke kuwa sina ugomvi na huyu miss TZ ila (je) bendera yetu inamjumuisha au inambagua? au tuna-assume au kufumba macho na kudhani iko sawa!!
..............................
..............................
*Sahihisho:
Serikali ya A. kusini inasema kuwa rangi ktk bendera yao ya Taifa hazina tafsiri yoyote (www.info.gov.za/aboutgovt/symbols/flag.htm).
"The national flag was designed by a former South African State Herald, Mr Fred Brownell, and was first used on 27 April 1994. The design and colours are a synopsis of principal elements of the country's flag history. Individual colours, or colour combinations represent different meanings for different people and therefore no universal symbolism should be attached to any of the colours."

No comments: