Jana mwanahabari mmoja (political editor) wa bbc bwana Nick Robinson aliniacha hoi!
Alikuwa akielezea kwenye tv kuhusu kupanda bei ya mafuta (fuel). Akaenda kituo cha mafuta, akachukua pampu na kuingiza katika tenki la gari yake huku akiendelea kulonga juu ya kupaa bei za mafuta kila kukicha!
Baada ya dakika moja hivi alirudisha pampu na kufunga kifuniko cha tanki.
Lakini cha ajabu muda wote huo jamaa akilonga maneno lukuki mita ya mafuta ilikuwa inaonyesha mafuta yanaingia ni lita 0.000 na bei ya mafuta yanayoingia 0.000, kilichokuwepo pale ni bei inaoonyesha kuwa lita moja ni kiasi fulani.
Kumbe alienda pale kuzuga tu!! Jamaa angesimama tu aseme maneno badala ya kuzuga kituoni kama vile anajaza mafuta kumbe anawakinga wenzake ambao walikuwa na shida ya kweli kujaza mafuta kwa pampu hiyo aliyoing'anga'ania muda wote huo.
Acha hizo Nick!! 'You have Been Framed'
.............................
Saturday, 28 June 2008
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment