Monday, 9 June 2008

Kandanda TZ!

Matokeo ya mechi za kimataifa nchini yanazidi kukatisha tamaa. Toka ngazi za vilabu hadi timu za Taifa tumekuwa hatufanyi vizuri kwa kipindi kirefu sasa.

Tatizo ni nini hasa.
Wataalamu tunawaleta sana tena kwa gharama kubwa, lakini bado tu. Tumejenga uwanja wa kisasa lakini bado.
Labda tatizo ni upeo wa uelewa wa wachezaji kimichezo na kisaikolojia - kwa maana kwamba wanahitaji kutoka nje (hasa nchi za ulaya) ili wachanganyike na wenzetu ili waweze kujifunza zaidi. Pia walimu wazalendo wawe wanapata kozi nje (ulaya).

Kwa hiyo serikali kupitia wizara ya michezo na utamaduni na shirikisho la kandanda waandae fungu maalumu la kuinua kandanda nchini kwa kuwatoa nje wachezaji na makocha ili waone na kujifunza zaidi.

No comments: