Baada ya jengo kuanguka wananchi wanajiuliza na kushindwa kujua lawama zimwendee nani.
Nitajaribu kufafanua juu ya kazi iliyopo ktk miradi mikubwa inayofanana na huu wa Jengo lililoanguka Kisutu, Dar, pamoja na wahusika ktk nafasi zao (nani ni nani ktk miradi kama hii).
Lengo langu sio kumnyooshea kidole yeyote aliyehusika ktk ujenzi wenyewe.
Wahusika wakuu ni kama ifuatavyo:
1. Mwenye jengo (client)
2. Msanifu/wasanifu wa jengo (designers -architect as head of the team)
3. Makandarasi (contractors -engineers)
4. Makandarasi wadogo (sub-contractors -engineers, materials suppliers etc.)
5. Mamlaka (wapitisha michoro na kutoa kibali)
6. Wananchi (Public as eventual users or neighbours)
Kazi ya mwenye jengo ni kutoa kazi (yeye ndiye mwenye mradi na anaulipia). Anamtafuta mtaalamu ili amfanyie kazi ili atimize ndoto yake kwa kumpa mahitaji yake mtaalamu au mtaalamu anamuandalia mahitaji client.
Mtaalamu ambaye anachukua jukumu la kutimiza ndoto ya mwenye jengo ni masanifu majengo (architect). Msanifu majengo anafanya uchambuzi wa mahitaji wa mwenye mradi (client) kwa kuzingatia uwezo wa kifedha wa client. Baada ya utafiti (analysis) msanifu majengo anamwendea mwenye mradi (client) na kumwonyesha mapendekezo (propasal) na makisio ya gharama (approximate estimats). Mwenye mradi akiyakubali mapendekezo, msanifu anaandaa michoro yote. Michoro husika ni ya kisanifu (architectural) na ya kihandisi (engineering drawings).
Kwa ufupi:
Architect ni mshauri wa mradi na anakuwa kiungo kati ya mwenye mradi (client) na wajenzi/makandarasi.
Architect anaandaa:
1. Brief (habari kuhusu mradi -site location, analysis (incl. soil investigation)
2. Michoro (architect and engineer/working drawings)
3. Schedules
4. Specifications of materials and workmanship
5. Cost estimates (Bill of Quantities)
6. Contract document
Baada ya hapo kinachofuata ni mchakato wa kutangaza tenda (tendering). Uchambuzi unafuatia kwa kuchagua kampuni itakayojenga mradi, na wakandarasi wadogo kama watahitajika kulingana na ukubwa wa mradi.
Kinachofuatia ni kutoa/kukabidhi mradi kwa mkandarasi aliyefuzu tenda (contract offer)
Hatua ya mwisho ni mradi kuanza (ujenzi).
Architect anakuwa ni mkaguzi wa maendeleo ya mradi. wakandarasi wao kazi yao ni kutumia michoro na vipimo (and specifications) viliyotayarishwa na architect ili kujenga jengo kama ilivyokusudiwa na mwenye mradi.
Jengo lililoanguka Dar
Tume iliyoundwa kwa msaada wa wataalamu (wasanifu majengo na wahandisi as expert witnesses) watachunguza hatua zote hapo juu na kuona kila mhusika kwa nafasi yake alitimiza wajibu wake ipasavyo.
Tume itachunguza michoro ya ujenzi na kulinganisha na ubora wa kazi yenyewe ya ujenzi kama ilifuata specifications zilizotolewa na wataalamu. (Kuanzia msingi wa jengo -aina na ujenzi wake, kuta, structural members, cement, sand, aggregates ratio etc.)
Itachunguza kama wahusika ngazi zote wana elimu na uzoefu unaostahili ktk ujenzi wa mradi huo (eneo la Kisutu, la ghorofa kumi, mali ya Kampuni ya McSon Investment Ltd)
Mamlaka husika kama zilipitia michoro na kutoa kibali cha kazi kwa uwazi na haki.
Kwa maoni yangu binafsi hayo ni baadhi ya mambo ambayo tume ya uchunguzi iliyoundwa na mkuu wa mkoa wa Dar itayapitia ktk kazi yake ya kutafuta chanzo na undani wa tatizo au matatizo yaliyosababisha tukio la kuanguka kwa jengo hilo la ghorofa kumi, mali ya Kampuni ya McSon Investment Ltd.
..................
(SOURCE: Alasiri, 2008-06-23 17:44:47. Na Sharon Sauwa, Jijini)
Juzi, mishale ya saa 4:00 na saa 5:00, jengo hilo la ghorofa kumi, mali ya Kampuni ya McSon Investment Ltd ambalo likuwa likijengwa na mkandarasi wa Kampuni ya N.K Decorators lilianguka na kuzua kizaazaa cha aina yake.
Katika tukio hilo, watu walioshuhudia walisema kuwa dalili za jengo hilo kutaka kuanguka, zilionekana tangu mapema na watu walipewa taarifa za kutoka.
Baada ya kuanguka, kazi ya ukoaji ilifanywa kwa kukishiriana na Jeshi la Wananchi wa Tanzania, Zimamoto na mgambo wa Jiji la Dar es Salaam.
Tayari Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Abbas Kandoro ameshaunda timu ya kuchunguza tukio hilo, ambayo imepewa wiki mbili kukamilisha kazi yake.
........................................................
Tuesday, 24 June 2008
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment