Wembe huu unaotumika kukimbizana na wauza bangi au wapika gongo utumike pia kuwashughulikia na kuwafikisha ktk mkondo wa sheria wezi wa mabilioni ya fedha za umma (mafisadi) ambao wanahusishwa na kashfa mbalimbali nchini!
Vyombo vya dola visiwe na mstari wa mbele tu kuwashughulikia hawa wananchi ambao wanasumbuliwa na umasikini, ambapo hela ambazo zingesaidia kuwanasua watanzania ili wasiuze bangi au gongo zimechukuliwa na wachache. Huyu mwananchi kama angekuwa na hela ya mkopo toka serikalini angefanya jambo la maana, lakini hela zenyewe serikalini zinaliwa na wachache (wenye uchu wa madaraka na utajiri); maskini wa watu anabaki njaa tupu na kuanza kuhangaika na maisha!
Nashangaa kweli!!
...........
...........
Mkazi wa Kisarawe akukutwa na bangi kilo saba!
(SOURCE: Alasiri, 2008-06-03 16:06:38. Na Sharon Sauwa)
Mkazi wa Kisarawe mkoani Pwani, William P.,38, anashikiliwa na Polisi kwa tuhuma za kukutwa na bangi kilo saba.
Kwa mujibu wa Kamanda wa Kikosi cha Kuzuia Madawa ya Kulevya Nchini, Godfrey Nzowa, mtuhumiwa alikamatwa kutokana na taarifa kutoka kwa wasamaria wema. Alikamatwa wakati akiziuza kwa wateja wake.
Atafikishwa mahakamani, wakati wowote upelelezi ukikamilika.
Tuesday, 3 June 2008
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment