Monday, 2 June 2008

Shirikisho A/Mashariki: Nionavyo III

Wakati nikitoa maoni yangu kipindi hicho, niliweza kuungwa mkono na watanzania wenzangu ktk nyakati tofauti. Kwa mfano ....
.....................
.....................
(at 06:25AM Tuesday on December 05, 2006, Dr.Khamis said):
Naunga mkono maneno ya Edison na wengineo wanaopinga “FEDERATION”. Sasa hivi kwenye Jumuiya YA Afrika ya Mashariki tuna,Tanzania,Kenya,Uganda,Rwanda na Burundi.
1. Tuwe na ushirikiano kwenye uchumi kama ule wa zamani, Bandari,Reli na Ndege.
2. Tushirikiane kuunda tena East African Airways na tuone kwamba tunafanikiwa sio kama sasa hivi kila nchi ina kampuni yake ya ndege.
3. Tujenge reli mpya na tuziimarishe reli za zamani ili usafiri wa mizigo na abiria uwe wa nafuu.Tukifanya hivi tutapunguza ajali za barabarani.

Nchi ambayo ni ya “amani” katika nchi hizi tano ni Tanzania pekee na kidogo Kenya. Historia ya Uganda ni vita, ya Rwanda ni vita na Burundi ni vita tu. Mpaka dakika hii hakuna Amani Rwanda,Burundi wala Uganda.
Hakuna “democracy” huko Uganda, Burundi wala Rwanda. Wengine wanataka kuwa Rais wa Maisha na kubadilisha katiba zao.
Federation itataka iwe na aina moja ya fedha(Monetary System) kama vile tunavyoona Euro currency katika EU –countries. Fedha ya Tanzania ni dhaifu sana.
Federation itataka iwe na jeshi moja,Bunge moja, serikali moja, rais mmoja tu.

Watanzania bado hatuko tayari na FEDERATION bali tuko tayari na muundo wa ushirikiano kama ule wa zamani wa JUMUAI YA AFRIKA YA MASHARIKI. Ni jukumu la serikali ya Tanzania kuwandaa watanzania kwa Federation. Mapaka muda huu Serikali ya Tanzania haijafanya matayarisho yoyote ya kuwaandaa wananchi wake katika hatua kubwa sana hii ya Federation.

No comments: