Hivi karibuni nilipata habari za kuporomoka kwa jengo refu la ghorofa 10 huko Dar (barabara ya Kisutu/Zanaki). Baada ya jengo kuanguka wananchi wanajiuliza na kushindwa kujua lawama zimwendee nani.
Nitajaribu kufafanua juu ya kazi iliyopo ktk miradi mikubwa inayofanana na huu wa Jengo lililoanguka Kisutu, Dar, pamoja na wahusika ktk nafasi zao (nani ni nani ktk miradi kama hii).
Lengo langu sio kumnyooshea kidole yeyote aliyehusika ktk ujenzi wenyewe.
Wahusika wakuu ni kama ifuatavyo:
1. Mwenye jengo (client)
2. Msanifu/wasanifu wa jengo (designers -architect as head of the team)
3. Makandarasi (contractors -engineers)
4. Makandarasi wadogo (sub-contractors -engineers, materials suppliers etc.)
5. Mamlaka (wapitisha michoro na kutoa kibali)
6. Wananchi (Public as eventual users or neighbours)
Kazi ya mwenye jengo ni kutoa kazi (yeye ndiye mwenye mradi na anaulipia). Anamtafuta mtaalamu ili amfanyie kazi ili atimize ndoto yake.
Mtaalamu ambaye anachukua jukumu la kutimiza ndoto ya mwenye jengo ni masanifu majengo (architect). Msanifu majengo anafanya kazi ya uchambuzi wa mahitaji wa mwenye mradi (client's requirements) kwa kuzingatia uwezo wa kifedha wa client.
Client anaweza kumpa architect mahitaji ya mradi wake (Client's Requirements) au architect anaweza kumwandalia mteja wake mahitaji hayo.
Baada ya utafiti (analysis) msanifu majengo anamwendea mwenye mradi (client) na kumwonyesha mapendekezo (sketchy propasals) pamoja na makisio ya gharama ya mradi (cost estimates). Mwenye mradi akiyakubali mapendekezo, msanifu anaandaa michoro yote.
Michoro husika ni ya kisanifu (architectural) na ya kihandisi (engineering drawings). Kazi hii inafanywa na timu ya wataalamu ktk fani ya majengo/ujenzi chini ya uangalizi wa msanifu majengo.
Kwa ufupi:
Architect ni mshauri wa mradi na anakuwa kiungo kati ya mwenye mradi (client) na wajenzi/makandarasi.
Architect anaandaa:
1. Brief (habari kuhusu mradi -site location, analysis (incl. soil investigation)),
2. Michoro (architect and engineer/working drawings),
3. Schedules,
4. Specifications of materials and workmanship,
5. Cost estimates (Bill of Quantities),
6. Contract document.
Baada ya hapo kinachofuata ni mchakato wa kutangaza tenda (tendering). Makampuni yanayopenda kujenga mradi husika yanatuma maombi kwa kufuata utaratibu uliotangazwa na mwenye mradi. Baada ya hapo uchambuzi unafuatia kwa kuchagua kampuni itakayojenga mradi (pamoja na wakandarasi wadogo kama watahitajika kulingana na ukubwa wa mradi).
Kinachofuatia ni kutoa/kukabidhi mradi kwa mkandarasi aliyeshinda tenda (contract offer)
Hatua ya mwisho ni mradi kuanza (ujenzi).
Kazi inapoanza architect anakuwa ni mkaguzi wa maendeleo ya mradi. Wakandarasi kazi yao ni kutumia michoro na vipimo (and specifications) viliyotayarishwa na architect ili kujenga jengo kama ilivyoonyeshwa ktk makubaliano (contract). Zaidi ya hapo kila asubuhi au kila wiki kunakuwa na mkutano ktk 'site' (site meeting) ili kujadili maendeleo ya Ujenzi wa mradi au matatizo yaliyojitokeza na kuyatafutia ufumbuzi. Mawasiliano yote kati ya wahusika yakuwa ktk maandishi (kwa kumbukumbu).
Kuhusu Jengo lililoanguka Kisutu, Dar
Tume iliyoundwa, kwa msaada wa wataalamu (wasanifu majengo, wahandisi, surveyors etc.), watachunguza hatua zote hapo juu na kuona kila mhusika kwa nafasi yake alitimiza wajibu wake ipasavyo.
Tume itachunguza michoro ya ujenzi na kulinganisha na ubora wa kazi yenyewe ya ujenzi kama ilifuata specifications zilizotolewa na wataalamu. (Kuanzia msingi wa jengo; type of foundation and contruction methodoly, kuta au structural members, cement-sand-aggregates ratios, etc.)
Tume itaangalia kumbukumbu za mawasiliano (nyaraka) kati ya wahusika kwenye ujenzi wa mradi.
Itachunguza kama wahusika ngazi zote wana elimu na uzoefu unaostahili ktk ujenzi wa mradi huo wa jengo (eneo la Kisutu, la ghorofa kumi)
Pia itachunguza kama mamlaka husika zilipitia michoro na kutoa kibali cha kazi kwa uwazi na haki.
Kwa maoni yangu, hayo ni baadhi ya mambo ambayo tume ya uchunguzi iliyoundwa na mkuu wa mkoa wa Dar itayapitia ktk kazi yake ya kutafuta chanzo na undani wa tatizo au matatizo yaliyosababisha tukio la kuanguka kwa jengo hilo la ghorofa kumi, mali ya Kampuni ya McSon Investment Ltd.
..................
Thursday, 26 June 2008
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment