Monday, 2 June 2008

Shirikisho A/Mashariki: Nionavyo IV

Tarehe 11/12/2006 nilihitimisha maoni yangu kwa kubashiri kuwa watanzania walio wengi hawalitaki shirikisho na kweli ndivyo ilivyotokea kuwa. Nikagusia matatizo ya Muungano wetu Bara na Zanzibar; na sasa imebainika ni kweli una mapungufu -angalia maendeleo ya mwafaka ...(soma zaidi hapo chini)!
.............
.............

(at 05:41AM Monday on December 11, 2006):
Wachangiaji wamekuwa wakitoa mapendekezo yao juu ya nini kifanyike. Ukipitia michango kadhaa utapata mapendekezo ya wachangiaji, tena wamependekeza mengi sana. Baadhi ya michango au mapendekezo ni kama ifuatavyo:
1. Jumuiya ya Afrika mashariki iendelezwe na kusaidiwa kikamilifu na nchi wanachama. Mchangiaji mmoja alisema yale mashirika ya jumuiya yarudi, bandari, reli, ndege n.k.
2. Fursa za SADC na COMESA zitumiwe kikamilifu.
3. Kero za muungano wa Tanzani Bara na Zanzibar zitafutiwe ufumbuzi haraka na kwa uwazi. Wazanzibari hawawezi kukubali kuingizwa katika muungano mwingine wakati huu tulio nao hawaufurahii hasa kutokana na mpasuko uliopo pamoja na kero zingine zilizopo ktk muungano wetu.

Tunaweza kuwa competitive ndani ya jumuiya yetu, au ktk SADC/COMESA. Pamoja na hayo, nchi zote za jumuiya ya Afrika Mashariki ziko ktk SADC/COMESA, je hilo shirikisho lina nini kipya?
Mwisho, sio kweli kwamba wakubwa wameshakubali au kupitisha shirikisho. Wananchi ndio tutakaoamua.
Nina imani kubwa watanzania walio wengi watakataa uundwaji wa shirikisho.
Jumuiya-YES, shirikisho-NO.

No comments: