Tuesday, 10 June 2008

Daladala wapandisha nauli kinyemela Dar!

Natoa rai kwa vyombo husika (viongozi SUMATRA) vifuatilie na kutafuta ufumbuzi kwa masilahi ya wananchi! Hii ni kero!

.................
(kutoka: Nipashe, 10/06/2008. Na Godfrey Monyo & Romana Mallya)
Uchunguzi umebaini kuwa, pesa zilizoongezwa katika nauli za sasa kwa baadhi ya daladala ni kati ya Sh. 50 hadi Sh. 200 wakati katika baadhi ya barabara kulikuwa na upungufu mkubwa wa magari ya abiria ikiwa ni matokea ya magari hayo kufanya kazi.

Baadhi ya daladala zinazofanya safari zake kati ya Mbagala rangi tatu na Mwenge zilipandisha nauli hadi kufika Sh. 600 wakati awali ilikuwa Sh. 350.

Aidha, magari yanayofanya safari zake kati ya Gongolamboto na Posta yalipandisha nauli hadi kufikia Sh. 500 badala ya Sh. 350.

No comments: