Serikali yetu ilipounda tume ya kukusanya maoni kuhusu mpango wa kuharakisha uanzishwaji wa Shirikisho la Afrika Mashariki, sikubaki nyuma ktk kuchangia maoni yangu. Mimi nilikuwa mmoja wa wananchi waliopinga uanzishwaji wa Shirikisho hilo.
Nilipata fursa kutoa maoni yangu ktk majukwaa mbalimbali.
Baadhi ya maoni niliyoyatoa ni kama ifuatavyo (yako ktk sehemu nne, na niliyatoa kupitia m/kijiji blog):
..............................
..............................
(at 10:34AM Monday on December 04, 2006, edison said):
Naunga mkono dhana ya ushirikiano kibiashara na kiuchumi kama ilivyo sasa na huko nyuma.
Hakuna haja kwa wakati huu kuanzisha shirikisho la kisiasa (rais mmoja na bunge moja).
Kwa kifupi siungi mkono "federation".
Kwanza sijui kuna vigezo gani vimewekwa na wahusika (au viongozi wa A. Mashariki) kwa kila nchi mwanachama wa Jumuiya, ili kujiunga na 'shirikisho!!!".
Haiwezekani eti kwa sababu za kijiografia tu ziwe kigezo cha kila nchi kujiunga.
Mimi nina vigezo vyangu binafsi, labda leo niongelee hivi vitatu kwa pamoja:
Utulivu, Amani na Demokrasia
Nchi pekee inayoweza ku'tick' all the boxes ni TZ tu.
Kenya demokrasia ni finyu sana na juzijuzi wameshindwa kutuletea wabunge 9 tu wa bunge la A. Mashariki na hadi sasa kesi iko mahakamani. Sasa wana ubavu wa kutoa wabunge wa bunge hilo la shirikisho? Tumeona hawana ubavu huo!! Uongozi wao si wa uwazi, tumeona mawaziri/manaibu waziri wanaachia ngazi. Hizo si dalili njema! Sera zao za ARDHI na Tanzania sio haziendani kabisa. WaTZ hatutaweza ku-access ARDHI yao kama watakavyoweza ku-access ARDHI yetu TZ!!!
VERDICT: Kenya haiwezi kujiunga ktk shirikisho.
Uganda: MUSEVENI AMEBADILI KATIBA YA NCHI ILI ATAWALE KWA VIPINDI KADRI ANAVYOJISIKIA (maisha?). Huu si mfano mzuri wa kukumbatia. Uganda kuna vita vya siku nyingi na Lord's Resistance Army na hatujui mustakabali wake! Hili tulifumbie macho na kumkaribisha Konyi na LRA ktk shirikisho, tutambebea mbeleko gani? Mgogoro Uganda na DRC umeishia wapi?
VERDICT: Uganda haistahili kujiunga.
Rwanda: Rekodi ya nchi hii kidemokrasia sio nzuri pia. Sina hakika Kagame ni mwanademokrasia halisi au ni mtu anayetabilika. Wamekuwa ktk vita kwa muda mrefu na tuhitaji muda kuona amani ya kweli ipo Rwanda.
VERDICT: TUNAHITAJI MUDA KUONA MAENDELEO YA AMANI NA DEMOKRASIA YA KWELI. It's a NO, for now!
Burundi: Ndio juzi juzi tu wametia saini makubaliano ya amani na PELIPEHUTU. Tunahitaji muda wa kutosha ku-assess maendeleo ya amani, usalama wa raia na ya demokrasia, pamoja na utekelezaji wa makubaliano yao. Pia tutahitaji ushahidi wa kututhibitishia kuwa silaha zote za kijeshi/kivita zimekabidhiwa kwa vyombo halali vya dola. Wapigaji wote wa msituni wakabidhi miundombinu ya kijeshi/kivita yote waliyo nayo ktk vyombo vya dola ili tuwe na imani juu ya usalama wa raia kwa sasa na siku zijazo na kudhibiti vitendo vya unyang'anyi, ujambazi wa silaha na ujangiri katika eneo la Jumuiya.
VERDICT: NI MAPEMA MNO kuiamini Burundi kama nchi iliyo na amani na demokrasia ya kweli. Hatujui kama hii amani ya sasa ni sawa 'volcano' hai, iliyolala au iliyokufa! I am afraid, it's a NO to Burundi.
Hizi ndio sababu zangu za kulikataa SHIRIKISHO kwa nguvu zangu zote. Ninazo sababu nyingi ila hizi ni za msingi kwangu. Athari zake (shikisho)zinaweza zisitupate sisi, ila vizazi vijavyo vinaweza kutulilia kama hatujali maslahi ya utaifa kwanza!!
NB:
Tusidanganyike kwa kiini macho cha Ajira, kwa hata kwa mazingira ya sasa (bila shikirikisho) ajira ni ngumu na sisi ndio nchi kubwa, mipaka ikiwa wazi wageni wataingia kwetu na kuua kabisa hii ajira iliyopo. Sera ya elimu na ardhi ya TZ ni nzuri kuliko nchi jirani, i.e. zinawajali wanyonge. Rwanda na Burundi kuna 'population density' kubwa sana, kwa hiyo watamiminikia TZ.
Shikisho litawanufaisha zaidi Kenya, Uganda, Burundi na Rwanda, kuliko waTZ tutakavyofaidika nalo. Tuta-loose wala hatuta-benefit a lot!
WAPO WACHACHE KTK TANZANIA WATAKAONUFAIKA SANA NA MUUNDO WA SHIRIKISHO. ILA WATANZANIA WALIO WENGI WATAPATA SHIDA SANA! Sasa lipi bora, wachache wapete na tuwaache wengi ktk shida?
Tusione haya wala aibu kusema 'NO' kwa muungano wa shirikisho! Muundo wa sasa WA JUMUIYA unatosha hasa ktk masuala ya kibiashara na kiuchumi!
Asante sana.
Monday, 2 June 2008
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment