Mawazo yangu;
-timu ijitegemee (kupitia vitega uchumi vyake vilivyopo na vingine vitakavyobuniwa.
-timu ijiendeshe kibiashara.
Utajiri wa timu umejificha ktk nembo ya timu (logo). Nembo ni alama ya timu, kwa hiyo ikisajiliwa na kutumika katika bidhaa za kibiashara mfano jezi (replica), nguo, mabegi, bendera ya timu n.k. timu itajiingizia hela nyingi za ziada. Hivi ndivyo timu kama Real Madrid na Manchester United zinavyojiingizia hela na kuwa vilabu tajiri duniani.
Pia timu inaweza kuomba mkopo kutoka ktk taasisi za kifedha ili kujenga uwanja wa kisasa wa kuchezea mechi zake za nyumbani ukiwa na huduma kama hoteli, vyumba vya kupangisha (ofisi/biashara) duka la bidhaa rasmi za timu (official club merchandise).
Timu ikionyesha bidii na ubunifu inaweza kuendelea. Uongozi/wanachama chagueni kuanza sasa mageuzi ya kimaendeleo kwa manufaa ya timu.
Friday, 1 February 2008
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment