Friday, 15 February 2008

Rais Jakaya Mrisho Kikwete wa Tanzania

Jina la Kwanza: Jakaya
Jina la Katikati: Mrisho
Jina la Mwisho: Kikwete

Chama: Chama Cha Mapinduzi (CCM)


Wasifu wa Rais Jakaya M Kikwete.
Alizaliwa Oktoba 7, mwaka 1950 katika kijiji cha Msoga Wilaya ya Bagamoyo mkoani Pwani.

Elimu.
1958-1961 - Shule ya Msingi Msoga
1962-1965 - Shule ya Msingi ya Kati ya Lugoba
1966-1969 - Shule Sekondari Kibaha
1970-1971 - Shule ya Sekondari Tanga
1972-1975 - Chuo Kiku cha Dar es Salaam, Shahada ya kwanza ya Uchumi
1976-1977 - Mafunzo ya Afisa wa Jeshi
- Mafunzo ya Uongozi wa Jeshi Monduli
1983-1984 - Mafunzo ya Makamanda wa Jeshi

Nafasi alizowahi kushika
1975-1977 - Katibu msaidizi wa TANU wa Mkoa
1977-1980 - Katibu Msaidizi wa CCM, Kisiwani Zanzibar
1980-1981 - Afisa Utumishi wa CCM makao makuu
1981-1983 - Katibu wa CCM Mkoa Tabora
1983-1986 - Mkufunzi wa Siasa katika Chuo cha uongozi wa Jeshi Monduli
1986-1988 - Katibu wa CCM Wilaya ya Nachingwea na baadaye Masasi
1988-1990 - Naibu Waziri wa Nishati na Madini
1990-1994 - Waziri wa Nishati, Madini na Maendeleo ya Maji
1994-1995 - Waziri wa Fedha
1995- 2005 - Mbunge wa Chalinze
1995-2000 - Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa
2000-2005 - Aliteuliwa tena kuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.
2005- Hadi Sasa - Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Maisha ya Binafsi:
Mheshimiwa Rais Jakaya M Kikwete ameoa na ana watoto kadhaa. Mke wake anaitwa Bi. Salma Kikwete. Mke wa Rais ni mwenyekiti wa taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA).

Nyongeza:
Mwaka 1995 mheshimiwa Rais Jakaya M Kikwete aligombea Urais na nusura apate nafasi ya kuwakilisha CCM ktk uchaguzi mkuu. Katika mwaka huo mheshimiwa Benjamin William Mkapa, Rais mstaafu, alipata nafasi ya kuwakilisha CCM ktk uchaguzi mkuu na hatimaye kushinda uchaguzi mkuu na kuwa rais wa awamu ya tatu.

No comments: