Waziri Mkuu mteule, Bw. Mizengo Pinda, alizaliwa mwaka 1948 huko Mpanda vijiji mkoa wa Rukwa. Yeye ni mtoto wa mkulima wa kawaida.
Alipata elimu hadi ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam ambako alitunukiwa shahada ya Sheria mwaka 1974.
Baada ya masomo yake alianza kazi kama wakili wa serikali katika Wizara ya Katiba na Sheria kazi aliyoifanya kwa miaka minne.
Baadaye aliitwa Ikulu ambapo alifanya kazi na awamu zote tatu za serikali kuanzia awamu ya kwanza.
Mwaka 1978 hadi 1982, Bw. Pinda alifanya kazi ofisi ya Usalama wa Raia, Ikulu na baadaye akafanya kazi kama Katibu Mnyeka Msaidizi wa Rais, kati ya mwaka 1982 na 1992
Mwaka 1996 alifanya kazi kama Katibu wa Baraza la Mawaziri nafasi aliyoishika hadi mwaka 2000.
Mwaka huo aligombea Ubunge Mpanda na kusinda.
Alizidi kujikita katika nafasi za kisiasa zaidi pale mwaka huo huo wa 2000 alipochaguliwa kuwa Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa) na mwaka 2006 alichaguliwa kuwa waziri kamili wa wizara hiyo.
* SOURCE: Nipashe, 09 Feb 2008
By Mwandishi Wetu
Saturday, 9 February 2008
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment