Tuesday, 12 February 2008

Baraza la Mawaziri

Rais JK ametangaza Baraza jipya la mawaziri, baada ya kuvunja baraza la mawaziri ya kufuatia Edward Lowassa kujiuzulu baada ya kukumbwa na kashfa ya Richmond.

Akizungumza katika ukumbi wa Tamisemi mjini Dodoma amesema baraza hilo limepunguzwa na kubakia na Mawaziri 26 badala ya 29 wa awali na Manaibu 21 badala ya 31.

(Menejimenti utumishi wa umma)
-Hawa Ghasia.

(Ofisi ya Rais muungano)
-Seif Mohamed Khatib.

(Mazingira)
-Batilda Burian.

(Ofisi ya waziri mkuu utaratibu wa bunge)
-Philipo Marmo.

(Tamisemi Tawala za mikoa na serikali za mitaa)
-Stephen Wasira,naibu Serena Kombani.

(Wizara ya mipango na Fedha)
-Mustafa Mkulo, manaibu Jeremia Sumari, Omari Yusuph Mzee.

(Afya na ustawi wa jamii)
-Prof Mwakyusa, Naibu Asha Kigoda.

(Ardhi Nyumba na maendeleo ya makazi)
-John Chiligati.

(Elimu na mafunzo ya ufundi)
-Prof Jumanne Maghembe, Manaibu Gaudensia Kabaka, na Mwantum Mahiza.

(Mawasiliano na Sayansi na Technologia)
-Shukuru Kawambwa Naibu Maua Daftari.

(Miundo mbinu)
-Andrew Chenge Naibu Milton Mahanga.

(Habari Utamaduni na Michezo)
-George Huruma Mkuchika, Naibu Joel Bendera.

(Kazi Ajira na maendeleo ya Vijana)
-Prof Juma Kapuya Naibu Ezekiel Chibulunje.

(Maji na Umwagiliaji)
-Mark Mwandosya, Naibu wake ni Engineer Christopher Chiza.

(Kilimo Chakula na Ushirika)
-Peter Msola, Naibu Mathayo David Mathayo.

(Maendeleo ya jamii Jinsia na Watoto)
-Magreth Sitta naibu Lucy Nkya.

(Maendeleo ya mifugo na uvuvi)
-Johhn Pombe Magufuli, Naibu DR. James Wanyancha.

(Maliasili na utalii)
-Shamsa Mwangunga, Naibu Ezekiel Maige.

(Mambo ya Ndani)
-Lawrence Masha naibu Hamis Kagasheki.

(Wizara ya Sheria)
-Mhe. Chikawe.

(Mambo ya nje na Ushirikiano wa kimataifa)
-Bernard Membe, naibu Seif Ally Idi.

(Wizara ya madini)
-Wiliam Ngereje, Naibu ni Adam Malima.

(Wizara ya Ulinzi)
-Hussein Ally Mwinyi, Naibu Emmanuel Nchimbi.

(Wizara Ya Afrika Mashariki)
-DR. E Kamala.

(Viwanda na Masoko)
-Mary Nagu naibu Cyril Chami.

Awali kabla ya kutangaza baraza hilo Rais Kikwete alisema kuna mawaziri walioomba kupumzika baada ya kutumikia serikali kwa muda mrefu na watabaki katika kushauri tu.
ambao ni Mzee Kingunge Ngombare Mwiru, na Joseph Mungai.

* SOURCE: Alasiri, 12 Feb 2008
By Mwandishi Wetu

No comments: