Nimeona picha ya mama Salma, mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ktk gazeti la Majira la leo 26.02.2008 nikafurahi sana.
Mama alikuwa akiongea na wananchi maeneo ya vijijini. Kilichonifurahisha zaidi ni jinsi alivyovalia mavazi ya kitanzania (kama mwanamama wa kawaida kabisa) na anavyoongea nao kwa ukaribu na kujichanganya. Nimevutiwa sana na jinsi anavyokuwa karibu na wananchi na kuwapa moyo na mbinu za kujikomboa kimaisha.
Hata taasisi yake WAMA nayo inafanya mambo mazuri kivitendo. Hongera sana mama Salma.
Tuesday, 26 February 2008
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment