Saturday, 2 February 2008

Maisha

Viongozi nchini kwetu wana mtihani mkubwa wa kuandaa mazingira ya watu hasa vijana kujitegemea kimaisha.
Kijana anapomaliza darasa la saba au kidato cha nne anakuwa hana mwelekeo kimaisha juu ya nini afanye baada ya masomo.
Ipo mianya mingi sana ya kumwendeleza kijana mfano michezo kama ajira - mpira wa miguu, tennis, riadha n.k. ni miongoni mwa waajiri wakubwa duniani. Nadhani mkono wa serikali kisera ni muhimu ktk kusaidia njia hii na wadhamini nao watusaidie kuinua sekta hii.
Kwa kweli vijana wanakosa kujiendeleza kimaisha kwa vile eti hawakupata ajira serikalini au sekta binafsi. Njia rahisi ni kujiajiri.
Kwa nchi zilizoendelea kujiajiri ni kuzuri sana.

No comments: