Friday, 30 November 2007

Yanga: Majina yaliyoenda CAF

Majina Yanga yatumwa CAF
Fomu za usajili wa wachezaji watakaochezea Yanga katika mashindano ya Kombe la Shirikisho mwakani jana zilitumwa katika Shirikisho la soka barani Afrika (CAF) kwa ajili ya kupata leseni.

Orodha hiyo ina majina ya wachezaji 27 na hivyo Yanga imebakisha nafasi tatu za usajili endapo itataka kuongeza hapo baadaye itakapokuwa imesonga mbele.

Wachezaji wa Yanga waliosajiliwa katika mashindano hayo ya kimataifa ni:

Ivo Mapunda, Benjamin Haule, Jackson Chove,
Amir Maftah,
Said Maulid,
Mrisho Ngassa,
Fred Mbuna,
Shadrack Nsajigwa,
Abuu Ntiro,
Abuu Ramadhani.

Credo Mwaipopo,
Gaudence Mwaikimba,
Waziri Mahadhi,
Nadir Haroub `Canavaro,
Vicent Barnabas,
Athumani Iddi,
Laurent Kabanda,
Aime Lukungu,
Samuel Ngassa,
Jerry Tegete.

Yanga itaiwakilisha nchi kwenye mashindano hayo kutokana na kufanikiwa kumaliza ligi ikiwa imeshika nafasi ya pili huku bingwa ambaye ni Simba itashiriki michuano ya Ligi ya Mabingwa wa Afrika na Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati.

* SOURCE: Nipashe, 30 Nov 2007
By Somoe Ng'itu

No comments: