Saturday, 3 November 2007

Nipashe na Katiba ya CCM!

Nadhani waandishi habari na wahariri wa gazeti Nipashe wamepitiwa kidogo kuhusu utaratibu wa CCM kupitisha maamuzi kwa kufuata katiba yao.
Gazeti la leo (Nipashe) linasema Kamati Kuu ya CCM imeteua majina ya wagombea nafasi uenyekiti na makamu (Zanzibar na Bara); na kwamba yanaenda moja kwa moja Mkutano Mkuu wa Chama.
Kiutaratibu yanatakiwa yapewe baraka na Halmashauri Kuu ya CCM (na ndivyo ilivyokuwa).
Hakuna sehemu yoyote ktk habari ya Nipashe ambapo kikao cha H/Kuu imetajwa.

Nimenukuu baadhi ya sehemu kutoka gazeti hilo:
'Kamati Kuu ilikutana katika kikao cha siri jana chini ya Mwenyekiti wake, Rais Kikwete kupitisha majina ya watu watakaogombea nafasi ya Umakamu Mwenyekiti wa CCM kutoka Tanzania Bara na Visiwani.
Wateule hao majina yao leo yatawasilishwa katika Mkutano Mkuu wa Uchaguzi tayari kwa kupigiwa kura.' - Nipashe 03/11/2007

Na Mosonga

No comments: