Saturday, 17 November 2007

Nguo za watoto rangi gani?

Kuna mazoea kwa wazazi wengi kuchagulia watoto rangi za nguo za kuvaa kulingana na jinsia zao. Mfano imezoeleka kuwa nguo za rangi bluu ni kwa mtoto wa kiume na pinki kwa wa kike.
Hivi karibuni wataalam kadhaa walikuwa na mjadala kuhusu hilo, ktk kipindi cha luninga 'the one show' (the 'beeb'). Wote walisema kuwa hakuna sababu yoyote ya maana zaidi ya mazoea na mtu anaweza kuvaa rangi yoyote bila kujali jinsia yake, watoto kadhalika!
Inaonekana hiki ni kitu cha kuiga tu, na inawezekana kuwa vipo vitu vingi tunaiga bila kujua vina uhalali au umuhimu gani kwetu na kimaisha kwa ujumla.

No comments: