Hongera sana waheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Jakaya Mrisho Kikwete, Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na M/kiti wa Baraza la Mapinduzi Amani Abeid Karume na Pius Msekwa kwa kuteuliwa kwenu kuwa wagombea wa nafasi za Mwenyekiti wa CCM, Makamu M/kiti Zanzibar na Bara.
Na Mosonga
MSEKWA ATEULIWA MAKAMU WA MWENYEKITI WA CHAMA CHA MAPINDUZI BARA
Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi imepitisha kwa Kauli moja jina la Mheshimiwa Rais JAKAYA MRISHO KIKWETE kuwa Mgombea Pekee wa nafasi ya Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi.
Halmashauri Kuu ya CCM imepitisha majina mawili katika nafasi ya Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara na Zanzibar.
Rais ABEID AMANI KARUME ameteuliwa kugombea nafasi ya Makamu Mwenyekiti wa CCM zanzibar na Ndugu PIUS MSEKWA ameteuliwa Kugombea nafasi ya Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara.
Wagombea wote watapigiwa kura leo kwenye Mkutano Mkuu wa CCM unaoanza leo Kizota nje kidogo ya Mji wa Dodoma.
Pia Halmshauri Kuu ilimteua Ndugu Khadija Faraji Kuwa Katibu wa CCM mkoa wa Unguja Kaskazini.
03 Nov 2007
From: www.ccmtz.org
Saturday, 3 November 2007
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment