Wakati wenzetu nchi zilizoendelea kama Uingereza na Marekani, viongozi wao wakuu au wagombea uongozi hukumbwa na kashfa za kutumia madawa ya kulevya na uvutaji bangi wakati wa ujana wao, sisi wabongo (waafrika) kashfa yetu kubwa inaweza kuwa wanawake au ukware!
Ni wasichana wangapi mtu amepitia? Ni wanawake wangapi umezaa nao watoto? Ni watoto wangapi umezaa nje ya ndoa? Au umeshatelekeza wanao, mkeo/wakeo?
Haya ni baadhi ya maswali ambayo yakijibiwa yanaweza kuibua kashfa na hata kumnyima mtu kura huko mbeleni.
Kwa upande wangu mie naomba kufanya 'dili' na 'totoz' wangu huko nyuma; chondechonde msiniangushe jamani. Hatukuachana kwa ubaya wowote eti??!! Na kwa bahati nzuri hakuna ka-mzigo nilikowaachia, au sio! Tubaki marafiki wa kawaida tu na tusaidiane kila mmoja anapokuwa mhitaji, kwani wote ni binadamu na makosa hayana mwenyewe!
Je kura yenu nimeipata au nimeikosa?
Friday, 30 November 2007
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment