Monday, 12 November 2007

rushwa ya ngono

Yapo makundi matatu ya ngono:
Ngono-hiarishwa, Ngono Hiyarishwa-Haramu na Ngono Haramu

Ngono-'Hiyari'shwa
Aina ya kwanza ya ngono hiarishwa ni ile ambayo ime'hiyari'shwa kidini, kimila au kisheria na wajamianaji wahusika wote wawili wanakubaliana.

Ngono 'Hiyari'shwa-Haramu
Aina ya kwanza ya ngono `'hiyari'shwa haramu` ni ile ambayo mjamiiaji mmoja (hasa wa kiume) anahiyarisha na mwingine (hasa wa kike) anakataa na kushurutishwa.

Ngono ya namna hii inatokea wakati wazazi wakitaka binti aolewe hata kama ni kinyume cha mapenzi ya huyo binti, kwa sababu mila inaruhusu na pia kuna manufaa wanayoyataka.
Aina hii ya ngono inamaanisha kwamba wazazi wanamshurutisha binti kwa sababu mila inaruhusu na kwa sababu wana manufaa ya kiuchumi.
Hii ina madhara ya kimaumbile na kihisia kwa binti anayehusika, na inapingana na mitazamo ya kisasa, haki za binaadamu na pengine sheria zinazopitishwa, hasa kwa sababu inawahusu mabinti ambao wanapaswa wawe masomoni badala ya kuozwa.
Ngono ya aina hii itaendelea kuleta utata, kwa sababu imo ukingoni mwa ngono 'hiyari'shwa na ngono haramu, kwa sababu kwa upande mmoja ime'hiyari'shwa na mila (kusudi kumnufaisha mzazi) lakini ni haramu kwa yule mshurutishwa kwa sababu anachukuliwa mateka.
Aina ya pili ya Ngono-'Hiyarishwa'-Haramu ni ngono ya shinikizo ambapo mjamiiaji mmoja (hasa wa kiume) anamshinikiza mjamiaji mwingine (hasa wa kike), kwa manufaa ya kuridhisha hisia na hamu zake huku yule mshurutishwa anaye'hiyari'sha ngono hiyo naye ana manufaa ya kibiashara.
Hii ndiyo inayoitwa -ngono ya rushwa-, kwa sababu kama ni kazi haajiriwi kazi hiyo kwa sababu ametimiza masharti ya ajira hiyo, lakini kwa sababu njia ya mkato imetumika.

Ngono-Haramu:
Ngono haramu ni ile ambayo mshurutishwa hahiari, wala haikubaliki kijamii, kibinafsi kisheria, kitamaduni wala kidini. Hii hupewa majina kama vile kubaka, kunajisi, na kadhalika.

By Anti Flora Wingia, 11 Nov 2007
Email: fwingia@yahoo.com

* SOURCE: Nipashe

No comments: