Thursday, 15 November 2007

Kwa nini madeni tusiyoyaweza?

Nimesoma hukumu kuhusiana na madai dhidi ya naibu waziri Mheshimiwa Fulani nimeshangaa.
Kwanza najiuliza ni kwa nini amejiingiza ktk deni kubwa kiasi hiki na wala (kwa maoni yangu) hakuwa na shida kubwa kimaisha, kama vile ugonjwa au dharura yoyote, ambayo imemlazimisha kuingia deni hilo!
Kusema ukweli, yeye kama waziri na ana uwezo kuendesha maisha yake ya kawaida bila kujiingiza ktk mkopo wa mamilioni ya hela!

Mimi binafsi naona hili liwe fundisho kwetu sote hasa watu wa kipato cha kawaida. Ni vizuri tukumbuke kutumia kwa uwiano na kiasi tunachopata au kuingiza.
Tujizuie na kujiingiza ktk bili za juu kuliko uwezo wetu au bila kuwa na mikakati ya kurejesha fedha za wale wanaotukopesha.

Unaona hata hela ya ada ya mwanae (Mheshimiwa ...) inadaiwa kuwa ni zaidi ya sh. 10,000,000/=.

'... pia anadai Sh.10,300,000 kama malipo ya gari pamoja na ada ya shule ya mtoto wa ....'
-Gazeti Nipashe, 15/11/2007.

'He further observed that the complainant had managed to get 500,000/-, being part of the alleged 10,300,000/- initial payment for the purchase of a new vehicle and school fees for defendant’s daughter'
-The Guardian, Thu 15 Nov. 2007.

Mi naona kiwango hiki ni kikubwa, hata kuliko kumsomesha mtoto Chuo Kikuu na kuhitimu shahada (kwa muda wa miaka mitatu).

Kwa wale tusio na uwezo mkubwa kifedha, tutumie shule na huduma za serikali ili kuepukana na kupatwa na hali kama hii!

Ni kweli kuwa wakati mwingine kutafuta msaada wa aina ya mkopo hakuepukiki, lakini pale pasipo na ulazima tujiepushe mzigo mzito wa madeni. Tukope kwa kadri ya uwezo wetu.

Kumbuka kukopa harusi kulipa matanga!!!

Na Mosonga

No comments: