Friday, 3 August 2007

Uteuzi H/Kuu CCM

03 Aug 2007By Lucy Lyatuu, Dodoma
Chama Cha Mapinduzi (CCM), jana kilitoa hadharani majina ya wanachama wake watakaogombea ujumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) kupitia makundi mbalimbali wakiwemo Bi. Rita Mlaki na Bi. Salome Mbatia ambao gazeti hili liliwaripoti kimakosa jana kwamba wameachwa.
Baadhi ya majina mashuhuri katika kundi la walioteuliwa kugombea Ujumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) CCM viti 20 Tanzania Bara ni pamoja na
Waziri Mkuu, Bw. Edward Lowassa,
Bi. Shy-Rose Bhanji,
Waziri wa Ulinzi, Profesa Juma Kapuya,
Naibu Waziri wa Miundombinu Dk. Milton Makongoro Mahanga,
Katibu Mkuu wa CCM, Bw. Yussuf Makamba na
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bw. Bernard Membe.

Wengine katika kundi hilo ni
Naibu Waziri wa Nishati na Madini Bw. William Ngeleje,
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Siasa) Bw. Kingunge Ngombale Mwiru,
Waziri Mkuu Mstaafu Bw. Frederick Sumaye,
Bw. Wilson Masilingi,
Bw. Filbert Bayi,
Bw. Abrahaman Kinana.

Wengine ni
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Bw. William Lukuvi,
Bw. Jaka Mwambi,
Naibu Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mshariki Bw. Deodarus Kamala,
Naibu Waziri wa Kilimo, Chakula na ushirika Bw. David Mathayo,
Bw. Aggrey Mwanri na
Bw. Isidore Shirima.

Wengine ni
Bw. Enock Chambili,
Bw. Christopher Gachuma,
Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Profesa David Mwakyusa,
Profesa Samwel Wangwe,
Waziri wa Miundombinu Bw. Andrew Chenge,
Waziri wa Kazi, Ajira na Maendeleo ya Vijana Bw. John Chiligati,
Brigedia Jenerali Hassan Ngwilizi na
Kapteni John Komba.

Wengine ni Bw. Novatus Makunga,
Bw. Tarimba Abbas,
Bw. Lucas Kisasa,
Bw. Job Ndugai,
Bw. George Simba Chawene,
Bw. Abdul Sapi,
Bw. Uhahula,
Bw. David Holela,
Bw. Stephen Wassira (Waziri wa Kilimo na Ushirika),
Bw. Emmanuel Mwambulukutu,
Bw. Amos Makalla,
Bw. Jackson Msomi,
Dr. James Msekela,
Bw. Mohamed Mkumba,
Prof Idris Mtulia,
Bw. Pascal Mabiti,
Bw. Said Fundikira,
Bw. Abeid Mwinyimusa,
Bw. Charles Kagonji na
Dk. Ibrahim Msengi.

Baadhi ya wanaogombea ujumbe wa NEC kupitia Vijana Bara ni
Bi. Zainabu Kawawa,
Bw. Nape Nnaunye,
Bw. Deogratias Ndejembi,
Bw. Paul Kirigiri,
Bw. Maghembe Maghembe,
Bi. Violet Mzindakaya,
Bi. Lucy Mayenga.

Ujumbe NEC Wazazi Tanzania Bara baadhi ya majina mashuhuri ni yafuatayo:
Bw. Enock Kalumuna,
Bw. Salim Tambalizeni,
Bw. Richard Hizza Tambwe,
Bw. Mustapha Yakub,
Bw. Mussa Hassan Zungu,
Bw. Ruth Msafiri, .....(bwana au bi?)
Bw. Thomas Ngawaiya,
Bw. Henry Shekifu,
Bw. Richarch Nyaulawa,
Bw. Danhi Makanga,
Bw. Dickels Shindika,
Dr. Zainabu Gama,
Bw. Adam Kighoma Malima,
Bw. Stella Manyanya na
Bw. Athumani Mfutakamba.

UWT Bara ni
Bi. Halima Mamuya,
Bi. Sifa Swai, Bi. Asha Baraka,
Bi. Khadija Kopa,
Bi. Jacqueline Liana,
Bi. Anne Makinda,
Bi. Jane Mihanji,
Bi. Fatuma Adam Mkwawa,
Bi. Rita Mlaki,
Bi. Sofia Simba,
Bi. Margaret Sitta,
Bi. Kate Kamba,
Bi. Shamsa Mwangunga,
Bi. Anne Kilango Malecela,
Bi. Salome Mbatia,
Bi. Zakia Meghji,
Dr. Rehema Nchimbi,
Bi. Halima Kihemba,
Bi. Margaret Mkanga,
Bi. Lydia Boma,
Bi. Esther Nyawazwa,
Bi. Zainab Vullu ,
Bi. Esha Stima,
Bi. Diana Chilolo,
Bi. Tatu Ntimizi,
Dr. Aisha Kigoda,
Bi. Mwantumu Mahiza na
Beatrice Shelukindo.

Taarifa hiyo inaonyesha kwamba wana-CCM
60 wameteuliwa kuwania nafasi ya ujumbe wa NEC Taifa kwa upande wa Tanzania Visiwani,
18 kupitia UVCCM,
12 kupitia Wazazi na
21 kupitia UWT.

Hali kadhalika, wana-CCM watano wameteuliwa kugombea nafasi ya Halmashauri Kuu ya Taifa kupitia mikoa mitano ya Zanzibar.

Hata hivyo, vigogo kadhaa wameamua kutangaza rasmi kung’atuka katika uongozi wa chama. Wana-CCM waliochukua hatua hiyo ni pamoja na
Dk. Chrisant Mzindakaya,
Bi. Maria Watondoha,
Balozi Isaack Sepetu,
Bw. Daniel Ole Njoolay,
Bw. Charles Keenja,
Profesa Philemon Sarungi,
Bw. Stephen Mashishanga,
Bw. Paul Kimiti,
Bi. Asha Makwega na
Bi. Shamim Khan.

Kadhalika, wapo wana-CCM kadhaa walioamua kujiengua na uongozi wa chama hicho katika nafasi za Uenyekiti wa Mikoa akiwemo Bw. Pancras Ndejembi (Dodoma).

Aidha, nafasi za ujumbe wa NEC kwa mikoa ya Mara na Katibu wa Siasa na Uenezi Mkoa wa Lindi, zitarudiwa kutokana na sababu mbalimbali.

Vile vile nafasi ya Katibu wa Siasa na Uenezi Mkoa wa Kaskazini Unguja, Mwenyekiti wa CCM Moshi Vijijini na Mwenyekiti CCM Wilaya ya Rungwe, zitarudiwa kwa sababu kama hizo.

* SOURCE: Nipashe

http://www.ippmedia.com/

No comments: